Mahakama ya Haki ya Uaya ECJ imetoa uamuzi wa kupiga marufuku vazi
lolote linalovaliwa kwa misingi ya kidini katika maeneo ya kazi. Amri
hiyo inajumuisha dini zote, ikihakikisha kuwa haibaguwi waumini wa dini
ya Kiislam, Sikhs na wengineo ambao wanaweza kuchagua mavazi kulingana
na miongozo ya kidini. Amri hiyo pia inazuia mavazi yoyote ya misingi ya
kisiasa au kifalsafa. Mashirika mengi ikiwamo Shirika la Kutetea Haki
za Binaadamu Amnesty International yamekosoa amri hiyo. Mahakama hiyo
yenye makao yake Luxembourg ilikuwa ikisikiliza kesi ya mwanamke wa
Kiislam aliyefukuzwa kazi na shirika la usalama la GS4 nchini Ubelgiji
baada ya kusisitiza kuvaa hijab akiwa kazini. Shirika la Amnesty
International limesema uamuzi huo wa mahakama ni wa kusikitisha na
utachochea ubaguzi katika maeneo ya kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment