TRA

TRA

Tuesday, April 18, 2017

Korea Kaskani yalaani Marekani kwa 'kuhujumu' amani

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Balozi wa Korea Kaskazini ameituhumu Marekani kuhujumu amani na utengamano katika Rasi ya Korea wakati mvutano ukishamiri katika eneo hilo. 

Akizungumza katika Umoja wa Mataifa Balozi Kim In-ryong alisisitiza kuwa Korea Kaskazini iko tayari kwa vita kamili na Marekani. 



 Alisema mwenendo wa Marekani wa kutumia ubabe kuzivamia nchi huru na baadaye kudai inachangia katika kulinda amani ya dunia ni kukosa uwajibikaji. 

Korea Kaskazini ambayo hujulikana pia kama Jamhuri wa Kidemokrasia ya Watu wa Korea ilizidisha mvutano wa kikanda kwa kufanya jaribio jingine la kurusha kombora ambalo lilishindwa Jumapili. 

Wanadiplomasia kadhaa wa nchi hiyo wamesema nchi yao itaendelea kufanya majaribio mengine kila wiki, kila mwezi na kila mwaka.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger