TRA

TRA

Tuesday, April 18, 2017

Uturuki yarefusha utawala wa sheria ya hali ya hatari

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Naibu Waziri Mkuu wa Uturuki Numan Kurtulmus amerefusha muda wa utawala wa sheria ya hali ya hatari kwa miezi mitatu zaidi, hiyo ikiwa mara ya tatu kurefusha kipindi hicho tangu jaribio la mapinduzi lililoshindwa Julai iliyopita. 

Hayo yanajiri siku chache baada ya kura ya maoni iliyopigwa Jumapili kuhusu mabadiliko ya katiba yatakayomuongezea madaraka Rais Recep Tayyip Erdogan.



             Rais Recep Tayyip Erdogan

Erdogan ambaye amezilaani nchi za Magharibi kwa kile alichokiita ''fikra za vita vya msalaba'' amesema mamlaka zaidi mikononi mwa rais ni muhimu kuweza kuendeleza utengamano. Kura hiyo ilimpa ushindi Erdogan na chama chake lakini chama kikuu cha upinzani kimetaka matokeo yabatilishwe kikidai upigaji kura wa Jumapili ulighubikwa na mizengwe.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger