TRA

TRA

Sunday, April 2, 2017

MAKAMU WA RAIS CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (DARUSO) SHAMIRA MSHANGAMA AKUTANISHA WADAU KUJADILI DHANA YA “MWANAMKE NA UONGOZI” UDSM

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


32
Aliyekuwa
Mgeni Rasmi katika kongamano hilo lililo andaliwa na Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa 
Chuo Kikuu cha Dar es salaam Bi. Shamira Mshangama Mh. Sophia Mjema
akitoa nasaha zake kwa wote waliohudhuria katika kongamano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Nkurumah Chuo kikuu cha Dar es salaam.
  Makamu
wa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam Bi.
Shamira Mshangama akieleza kwa ufupi juu ya Kongamano hilo na
Kumkaribisha Mkurugenzi wa Maswala ya Jinsia Chuo Kikuu Cha Dar es
salaam Dkt. Kafanabo

Mkurugenzi wa Maswala ya Jinsia Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt.
Kafanabo akielezea kwa undani juu ya jinsia na uongozi katika kongamano
hilo
 Mkurugenzi
Mkazi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) nchini
Tanzania Bi. Martha Nghambi akielezea shughuli za asasi hiyo na nafasi
ya mwanamke katika uongozi.
Meneja
wa Benki ya NMB PLC tawi la Chuo Kikuu cha Dar es salalaam Bi. Rehema
Mwibura akielezea safari yake ya uongozi mpaka hapa alipofikia sasa na
kuwaatha vijana wakike wasikate tamaa kwa kuwa wanaweza.
 Mwanachama
wa zamani wa USRC Bi. Yunge Kanuda akiwasihi vijana wanawake kuwa
wanayo nafasi ya kugombea ngazi mbalimbali za uongozi hivyo wanatakiwa
wathubutu ili waweze kushika nyadhifa mbalimbali.
Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia kwa makini mijadala mbalimbali inayoendelea
Aliyekuwa Spika wa Bunge la USRC kwa mwaka 2014/2015 Protus Petro akielezea juu ya uongozi 
Aliyekuwa
Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Irene Ishengoma na aliyeshiriki Shindano la Maisha Plus 2016 akielezea
mambo mbalimbali yanayowahusu wanawake na kuwasihi kuto bweteka kwa kuwa
wanaweza.
 Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo wakiuliza maswali na kuchangia mawazo katika Kongamano hilo.
 Mwanzilishi na Rais wa Taasisi ya wanafunzi wanawake kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Consolata Chikoti akifuatilia kwa makini mijadala ikiendelea.
 Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema (wa nne kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na waliokuwa wazungumzaji wakati wa Kongamano hilo.
  Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Kongamano la Wanawake na Uongozi
  Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema (wa nne kutoka kushoto) kwa waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi wa Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Dar es salaam.
 Picha ya pamoja ya viongozi kutoka maeneo mbalimbali ikiwa ni Asasi,vyuo na shule shule mbalimbali
Washiriki wakiwa katika Kongamano hilo.
Picha zote na Fredy Njeje
 

Na
Dickson Mulashani
Makamu
wa Rais wa Serikali ya wanafunzi katika Chuo kikuu cha Dar es salaam Bi.
Shamira Mshangama, aliandaa kongamano kubwa lililohusisha watu mbalimbali
wakiwemo wanafunzi kutoka shule za Sekondari,wanavyuo,taasisi na asasi za
kijamii kwa lengo la kuzungimzia masuala mbalimbali yanayowahusu vijana hasa
vijana wa kike na dhana ya uongozi ikiwa ni pamoja na nafasi ya mwanamke katika
uthubutu wa kuwa katika nafasi mbalimbali za uongozi.
Akizungumza
katika kongamano hilo mgeni Rasmi katika ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.
Sophia Mjema aliwaeleza washiriki wa kongamano hilo safari nzima ya maisha yake
katika uongozi lengo likiwa kuwapa mwanga kuwa wanawake wanaweza kushika nafasi
mbalimbali bila wasiwasi.
Mh.
Sophia aliwaatha vijana hasa wa vyuoni na mashuleni kuto danganyika na kutoa
rushwa ya ngono na kuto kujirahisiha maeneo ya kazi ili mtu fulani ampende
amchukue ili apate kitu fulani na kusisitiza kuwa hayo ni mambo yanapita na waepuke
tamaa hizo.
Kadhalika
aliongeza kuwa kwa wanawake wote ambao wanania ya kugombea nafasi kama Ubunge
pindi wanapopata wawe mbele zaidi katika kutetea maslahi ya wanawake kwa kuwa
wao wanaona mambo mengi zaidi katika jami.
Mwisho
alisisitiza kuwa mambo yote yanawezekana endapo amani itadumishwa katika eneo
la kazi kwa kuwa sehemu ambayo haina amani hata utendaji wa kazi huwa ni mgumu,
alisema kuwa watu wakipendana na swala zima la kazi litakuwa na ufanisi
zaidi.     
Kwa
upande wake Mkurugenzi mkazi wa Asasi ya kiraia ya Global Peace Foundation
(GPF) Martha Nghambi alielezea kwa undani kuwa ” GPF ni ni Taasisi isiyo
ya kiserikali,ambayo si ya kidini na haitengenezi faida ya aina yoyote ile ina
makao yake makuu  katika jiji la
Washington DC nchini Marekani na lenye matawi yapatayo 23 duniani kote,
yakiwemo mabara ya Afrika,Ulaya, Asia na Marekani ni “Taasisi hii kwa Tanzania
ilianzishwa kati kati ya Mwaka juzi 2015 ambapo pamoja na uchaga wake
wameonesha juhudi kubwa katika kuhamasisha amani nchini kuanzia ngazi ya
familia na jamii kwa ujumla.”
Mathalan
Mkurugenzi huyo akiongelea umuhimu wa wanawake katika nafasi mbalimbali za
uongozi aliwasihi vijana wakike tangu wakiwa wadogo wawe na watu ambao ndio
mfano kwao “Role Model” watakao wafanya kutimiza ndoto zao, pia kuwa
na uthubutu kwa kuwa wanaweza kushika nyadhifa mbalimbali kuanzia ngazi ya
chini mpaka uongozi wa juu.
Nae
Mkurugenzi wa  wa Maswala ya Jinsia Chuo
Kikuu Cha Dar es salaam Dkt. Kafanabo pamoja na kutoa ufafanuzi wa historia za
viongozi wanawake waliowahi kushika nyadhifa mbalimbali nchini Tanzania alisema
kuwa nia ya wanawake katika uthubutu wa katika kutafuta nafasi mbalimbali bado
hauridhishi kwani safari ya kupambana na mfumo dume hata kwa wanawake wasomi
bado ni ndefu

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger