MULTICHOICE KUTUNUKU WATEJA WA
DStv CHANELI ZA BURE
Kampuni ya Multichoice imetangaza kuanzisha programu mpya ya kuwatuza wateja wake wa DStv kwa kuwaongezea chaneli mpya kwenye vifurushi vyao bila malipo yoyote ya ziada.
Kampuni ya Multichoice imetangaza kuanzisha programu mpya ya kuwatuza wateja wake wa DStv kwa kuwaongezea chaneli mpya kwenye vifurushi vyao bila malipo yoyote ya ziada.
Programu hiyo ijulikanayo kama -
DStv THANKS – imezinduliwa lea na ni mahsusi kuwashukuru wateja
wake ambao wamekuwa wanatumia huduma za DStv kwa muda wa miezi mitatu
mfululizo au zaidi.
Wateja
hawa watapata zawadi ya kuongezewa Chaneli nne mpya kwenye vifurushi
vyaozikiwemo zile za tamthilia, sinema, elimu, sanaa na
vichekesho. Chaneli hizo ni pamja na ile maarufu ya sinema za kihindi
ijulikanayo kama
Zee Bollymovies itakayo patikana DStv chaneli 114.
Chaneli hii itakuwa na sinema za kihindi za zamani pamoja na zile za kisasa kama vile
Mohra, Kushi, na Fitoor.
Chaneli nyingine itakayotolewa kama zawadi kwa wateja ni Viasat Life
itakayoonekana DStv chaneli 177. Hii imesheheni
burudani, wasifu wa watu wa kawaida ambao waliweza kufanya mambo
makubwa pamoja na mambo mengi ya maisha ya kila siku huku ikibeba
vipindi kama vile
Martha & Snoop’s Potluck Dinner Party, ‘The Rock’, Wake Up Call, House of Curves,
The Three Day Nanny na My Floating Home.
Nina TV itakayoonekana
DStv chanel 143 ni maarufu kwa tamthilia zikiwemo zile za Kiafrika na za Amerika Kusini. Pia Chaneli ya
Trigger itakayoonekana DStv chanel 188 nayo pia itatolewa kama sehemu ya zawadi kwa wateja wa DStv.
Kwa
kuanzia Tarehe 7 hadi 21 mwezi huu, wateja wote wa DStv watapata
chaneli hizo na baada ya hapo zitaendelea kubaki
kwa wateja ambao wametumia mfululizo huduma za DStv kwa miezi mitatu na
zaidi. Kila mteja anayefikisha miezi mitatu ya kutumia mfululizo huduma
za DStv atakuwa anapata chaneli hizo za ziada bila akujali aina ya
kifurushi anachotumia.
Akizungumzia
programu hiyo ya kuwazawadia wateja, Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice
Tanzania Maharage Chande amesema
“Tunafurahi sana kuzindua programu hii mahsusi ya kuwashukuru wateja
wetu. Ni dhamira yetu endelevu kuwaheshimu na kuwathamini wateja wetu
kwa dhati, hii niyo sababu kubwa inatufanya tuwape fursa hii adhimu ya
kuweza kufurahia zaidi huduma zetu.” Alisema Maharage
na kuongeza kuwa Multichoice itaendelea kuhakikisha kuwa huduma za DStv
zinaendelea kuboreshwa na kufikishwa kwa wananchi wengi zaidi ili
waweze kufurahia maudhui yaliyomo kuanzia michezo, burudani, habari,
elimu na hata chaneli za kidini pia.
Mkurugenzi
huyo amesema mbali na kuwajali wateja wake, Multichoice pia inaendelea
na programu zake nyingine
za kijamii kwa lengo lilelile la kuchangia kikamilifu katika maendeleo
ya kijamii na kiuchumi hapa nchini. Ameahidi kuwa mwaka huu 2017,
Multichoice imejipanga kuendelea kushiriki katika kuimarisha michezo,
taaluma na ubunifu
Kampuni
ya Multichoice Tanzania imekuwepo hapa nchini kwa takriban miaka 20
sasa na imekuwa kinara katika huduma za ving’amuzi ambapo king’amuzi
chake cha DStv kimekuwa
maarufu na kutumika kila pembe ya nchi hadi vijijini.
SHARE
No comments:
Post a Comment