Meneja
Kitengo cha Kumaliza Malaria Zanzibar Mwinyi Issa Khamis akijibu
maswali ya waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya malaria
yaliyoadhimishwa kwa mkutano wa waandishi wa habari Wizara ya Afya
Zanzibar.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Mkurugenzi
Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt, Fadhil Mohd Abdalla akimkaribisha
Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman kuzungumza na waandishi wa
habari katika maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani katika ukumbi wa
Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Naibu
Waziri wa Afya Zanzibar Bi. Harusi Said Suleiman akizunguza na
waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya Malaria Dunia katika
ukumibi wa mikutano wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Mwandishi
wa habari wa ITV/Radio One Farouk Karim akiuliza swali katika
maadhimisho hayo yaliyofanyika kwa mkutano wa waandishi wa habari katika
Wizara ya Afya Mnazimmoja.
NA
RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR
NAIBU
Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman amesema pamoja na mafanikio makubwa
katika kupambana na Malari Zanzibar, bado shehia tano zinaendelea kutoa
wagonjwa wa maradhi hayo zaidi ya asilimia tano.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya Malaria Dunia katika
ukumibi wa mikutano wa Wizara ya Afya Mnazimmoja, amezitaja shehia hizo kuwa ni
Tumbatu Jongowe, Miwani, Micheweni, Chukwani na Kiwengwa.
Hata
hivyo amesema maambukizi ya malaria katika maeneo hayo yanasababishwa na
wasafiri wanaoingia na kutoaka nje ya Zanzibar mara kwa mara ambapo mwaka jana
asilimia 55 ya wagonjwa waliogundulika walikuwa na tabia hiyo.
Amesema
takwimu za Malaria Zanzibar zinaonyesha mafanikio mazuri ambapo mtu mmoja kati
ya watu mia moja hupata ugonjwa huo katika jamii isipokuwa shehia hizo tano.
Naibu
Waziri wa Afya amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na
Malaria ikiwemo kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa na kusafisha mazingira kwa
lengo la kuondosha mazalio ya mbu wanaoeneza maradhi hayo.
Ameongeza
kuwa Serikali kwa upande wake mwaka jana iligawa vyandarua 705,000 bila malipo
na kufanya zoezi la kupiga dawa nyumba za wananchi ya kukinga malaria bila ya
kuangalia vyeo vya wamiliki wa nyumba hizo licha ya kukabiliana na changamo
nyingi katika kazi hiyo.
Amesema
baadhi ya wananchi wamekuwa wakikataa kupigiwa dawa nyumba zao kwa madai kwamba
zinawaletea athari za afya jambo ambalo halina ukweli kwani dawa hiyo ni salama
kwa afya.
Amekubusha
kuwa Sheria ya Afya ya Jamii na Mazingira ya mwaka 2012 pamoja na mambo mengine
inasisitiza juu ya udhibiti wa mbu na mazingira hivyo wananchi watakaokataa
kupigiwa dawa sheria itawabana.
“Watu
wanaokataa nyumba zao kupigiwa dawa ya kukinga maluaria bila sababu za msingi
zinazokubalika, sheria hii itawabana na hatua muafaka zitachukuliwa dhidi yao,
” alisisitiza Naibu Waziri.
Meneaja
Kitengo cha kumaliza malaria Mwinyi Khamis alisema Zanzibar imeweka mikakati ya
kumaliza kabisa malaria ifikapo mwaka 2023 hivyo juhudi za jamii na Wizara ya
Afya ni muhimu.
Amesema
mwaka jana watu watano walibainika kufa kwa malaria Zanzibar wakiwemo watoto
wawili wenye umri chini ya miaka mitano.
Mapema
akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Dkt.
Fadhil Mohd amewashauri wananchi wasikubali kula dawa ya malaraia bila kupimwa
na kuthibitishwa kuwa wanayo malaria.
Kauli
mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu inasema Malaria bado ipo Zanzibar, chukua
tahadhari.
SHARE
No comments:
Post a Comment