NA K-VIS BLOG NA MASHIRIKA YA UMMA
JESHI
la Marekani, limedondosha bomu kubwa lililopewa jina “Mama wa mabomu yote”
kwenye mapango ya wapiganaji wa Kiislamu wa ISIS hulo Afghanistani Aprili 13,
2017.
Bomu
hilo lijulikanalo kama GBU-43/B ni bomu lenye nguvu kubwa lisilo la kinyuklia
kuwahi kudondoshwa katika karne hii na linaweza kufanya uharibifu kwenye eneo
la ukubwa wa yadi 1,000
Rais
wa zamani wa Afghanistan, Hamid Karzai, amelaani shambulio hulo na kuwataka
Waafghani waamue wenyewe kama bado wanahotaji usaidizi wa Marekani nchini mwao
kwani ilivyo sasa, Marekani imeamua kuitumia nchi hiyo kufanya majaribio ya
sikaha zake.
Kwa
mujibu wa wizara ya Ulinzi ya Marekani PENTAGON, shambulio hilo kubwa kufanywa
chini ya utawala wa Rais Donald Trump.
Rais
Trump alisema, “Niliamuru majeshi yangu baada ya kikao kazi cha dharura
Ikulu na kuita bomu hilo ni mafanikio
mengine makubwa yaliyotekelezwa na majeshi yake.” Alisema.
SHARE









No comments:
Post a Comment