NA
K-VIS BLOG
POLISI
wanaokadiriwa kuwa watano wameuawa katika shambulio la kuvizia wilayani Kibiti
mkoa wa Pwani, Aprili 13, 2017.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amethubitisha kutokea kwa tukio
hilo lakini hakutaja idadi kamili ya askari polisi waliouawa.
“Ni
kweli askari wetu wanaokadiriwa kuwa watano, wakiwa katika gari lao la
doria,
wakitoka eneo la Jaribu Mpakani kurejea Kibiti walishambuliwa kwa risasi
na watu wasiojulikana na gari lao likapinduka lakini bado
sijapata idadi kamili ya waliouawa.” Alisema.
Waziri
Nchemba alisema, kimsingi shambulio hilo wanalichukulia kama ni kulipiza kisasi
kwa wahalifu hao dhidi ya askari polisi ambao wamekuwa wakifanya kazi nzuri ya
kuwadhibiti wahalifu hao ambao kwa sasa wanatafuta mahala pa "kujificha" mkoani
Pwani baada ya kufurushwa jijini Dar es Salaam.
Waziri
amesikitishwa na shambulio hilo na kuwataka Watanzania kuwa watulivu wakati
jeshi la polisi linaendelea na operesheni ya kuwasaka wahalifu hao ambapo
aliongeza kuwa taarifa kamili ya tukio hilo baya, itatolewa na Kamanda wa
Polisi Mkoani Pwani leo Aprili 14, 2017.
Kumekuwa
na matukio ya polisi na watumishi wa serikali kushambuliwa na wahalifu mkoani
Pwani ambapo tukio la hivi karibuni kabisa, polisi walimuua mwanamume mmoja
aliyejaribu kuwatoroka polisi akiwa amevalia vazi la hijab linalovaliwa na
wanawake.
SHARE
No comments:
Post a Comment