Mtoto mchanga wa siku nne ni miongoni mwa zaidi ya wahamiaji 480
waliookolewa na meli za uokozi katika Bahari ya Mediterania katika
operesheni za kuwatafuta na kuwaokoa wahamiaji waliokwama baharini.
Mtoto huyo alikuwa akisafiri katika boti mbili zilizokuwa zimewabeba wahamiaji kutoka nchi za kaskazini na kati ya Afrika, Sri Lanka na Yemen.
Mama wa mtoto huyo raia wa Nigeria na mumewe raia wa Ghana pia waliokolewa katika operesheni hiyo iliyofanywa na shirika lisilo la serikali la Uhispania Proactiva Open Arms.
Waliokolewa wanatarajiwa kuwasili katika kisiwa cha Sicily. Kiasi ya wahamiaji 600 wamekufa maji wakijaribu kufika barani Ulaya.

No comments:
Post a Comment