Takriban waandamanaji 30 wa upinzani wametiwa mbaroni katika
maandamano ya kupinga rushwa mjini Moscow, Urusi.
Wizara ya mambo ya
ndani ya Urusi imesema wanaharakati hao wanashikiliwa kwa madai ya
kuvuruga utulivu wa umma wakati wa maandamano yasiyo na mamlaka.
Maandamano hayo ya jana yaliyohudhuriwa na watu 100 - yalikuwa madogo
kwa idadi ikilinganishwa na maandamano ya kupinga serikali ya wiki
iliyopita, ambayo yanatajwa kuwa ni makubwa zaidi katika kipindi cha
miaka mitano.
SHARE
No comments:
Post a Comment