TIMU ya taifa ya vijana ya Tanzania,
Serengeti Boys, wameonyesha maajabu baada ya kusawazisha mabao 2 katika dakika
10 za mwisho wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kujipima nguvu dhidi ya timu
ya soka ya taifa ya vijana ya Ghana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam, leo Aprili 3, 2017.
Ghana walianza kupata mabao yao mapema
kupitia Sulley Ibrahim kabla ya Arko Mensah kuongeza la pili.
Hadi dakika za nyongezwa zinaonyeshwa,
Serengeti ilikuwa nyuma kwa mabao mawili.
Lakini dakika ya 90+5, mshambuliaji
hatari wa Serengeti Boys, Assad Juma akafunga bao la mkwaju wa penalti baada ya
beki wa Ghana kuunawa mpira eneo la hatari.
Dakika ya 90+10, Muhsin Malima
akavunja mtego wa kuotea na kumalizia kazi nzuri ya kiungo wao.
Bao hilo liliamisha shamrashamra
uwanjani hapo na ikaonyesha kweli Boys wanastahili kuchangiwa, wanastahili
kuandaliwa ili wakafanye vizuri nchini Gabon katika michuano ya Kombe la
Mataifa Afrika.
|
No comments:
Post a Comment