Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu ya Halotel Le
Van Dai akibadilishana hati za makubaliano na Kaimu Mkuu wa Akiba za
Watu Binafsi wa Benki ya NMB, Boma Raballa ambapo wateja wa Halotel
watafaidika na huduma za kifedha za Halopesa kwa ataweza kuchukua na
kuweka fedha zake kutoka katika akaunti yake ya NMB. Makubaliano hayo
yalifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Ofisa Mwendeshaji wa
Halopesa, Henry Mavula na kulia ni Meneja wa Huduma za Ziada wa benki ya
NMB,Stephen Adili.
KATIKA kufanikisha azma ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa wananchi wenye vipato tofauti, kampuni ya mawasiliano ya Halotel na benki ya NMB zimeingia katika ushirikiano utakao wawezesha mamilioni ya watanzania kunufaika na huduma za kifedha nchi nzima.
KATIKA kufanikisha azma ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa wananchi wenye vipato tofauti, kampuni ya mawasiliano ya Halotel na benki ya NMB zimeingia katika ushirikiano utakao wawezesha mamilioni ya watanzania kunufaika na huduma za kifedha nchi nzima.
Hatua hii itawawezesha watanzania wengi
zaidi kufikiwa na huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ikiwa ni sehemu ya
kufanikisha azma ya serikali ambayo inazitaka taasisi mbalimbali za kifedha
kuwafikia wananchi na huduma zao hasa kwa maeneo ya vijijini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Le Van Dai amesema kuwa ni hatua
nyingine kubwa katika utoaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi
ambapo sasa huduma ya Halopesa itakuwa imeunganishwa na benki ya NMB ili
kuwawezesha wateja kufanya miamala kwa urahisi zaidi.
Dai ameendelea kuwa ushirikiano huo,
umeunganisha taasisi kubwa zenye wateja wengi na zilizosambaa kwa kiasi kikubwa
nchini. Tunatarajia huduma hii itapunguza kadhia kwa watumishi wa taasisi za
umma, wakiwemo walimu na watu wa sekta zingine wakiwemo wakulima, wavuvi na
wafanya biashara wanaoishi vijijini ambako huduma za kibenki hazijafika
kote. Maeneo haya kwa kiasi kikubwa hutegemea njia ya simu za mkononi kuweza
kutoa fedha au kuweka kwa njia ya haraka na usalama zaidi.
“Ushirikiano huu ni wa kipekee katika
kurahisisha maisha ya watanzania ambao wamekuwa wakipata tabu kupata huduma za
kifedha kutokana na maeneo wanayoishi. Sisi kama Halotel hadi sasa tumewafikia
watanzania kwa zaidi ya asilimia 95. Hivyo ni dhahiri kwamba wateja
watakaojiunga nasi wataweza kutoa au kuweka fedha huko huko waliko kupitia kwa
mawakala wetu ambao wameenea nchi nzima,” aliongezea Dai.
“Tunatambua
changamoto ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiwasibu Watanzania hasa wa
kipato cha chini. Kwani wengi wao walikuwa wanakwama kuweza kupata huduma za
kifedha kutokana na miundombinu kutowafikia. Mpaka hivi sasa Halotel ina
mawakala zaidi ya 30,000 walioenea nchi nzima. Hii itawawezesha wakazi wa
maeneo ambayo hayakuwahi kuwa na mawasiliano kabisa au huduma za kibenki sasa
kuweza kupata huduma za kifedha kupitia simu zao za mkononi,” alimalizia Naibu
Mkurugenzi wa kampuni hiyo.
Kwa
upande wake Kaimu Mkuu wa Huduma Binafsi za Kibenki wa NMB, Boma Raballa, amesema
ushirikiano huo ni mafanikio mengine makubwa ya kibiashara kwao hususani katika
kupanua wigo wa huduma zake na namna itakavyoweza kuunganisha teknolojia ili
kuwarahisishia watanzania kupata huduma za kifedha popote walipo.
“Benki ya NMB ni ya kwanza kutoa huduma
za kipekee na zenye ubunifu wa hali ya juu na tunaamini ushirikiano huu
utatuwezesha kuwafikia watanzania wengi zaidi. Watanzania wanahitaji huduma za
kifedha muda wowote na mahali popote walipo. Hivyo kuja kwa ushirikiano huu
kutawaletea uhakika wa kupata fedha tena kwa njia rahisi kabisa kwa kutumia
simu zao za mkononi maana sio muda wote watakuwa karibu na mashine zetu za
kutolea fedha (ATM) au matawi ya benki yetu,” alisema Raballa
“Kwa kushirikiana na Halotel tunaamini
tutakuwa tumefanikisha lengo la serikali na benki yetu kwa ujumla katika
kuwafikia watanzania wengi zaidi. Hii inamaanisha kuwa wateja wa kampuni hizi
mbili ambazo hawajafikia na huduma aidha za NMB au Halotel basi watafikiwa kwa
pamoja. Mbali na kurahisisha huduma lakini pia itasaidia kwa kiasi kikubwa
kurahisisha kuboresha na kurahisisha hali ya maisha na uchumi kwa watanzania,
yaani kwa watoa na wapokea huduma,” aliongezea Raballa.
SHARE
No comments:
Post a Comment