Taasisi
ya utafiti ya Gallup yenye makao yake makuu mjini Washington Marekani
imetangaza habari ya kuongezeka idadi ya wananchi wa nchi hiyo walio na
wasiwasi wa kupanda kiwango cha ukata hasa kati ya watu wa pato la chini
na tabaka la watu masikini nchini humo.
Uchunguzi
wa maoni uliofanywa na taasisi hiyo kuanzia tarehe mosi hadi tarehe
tano mwezi uliopita wa Machi unaonesha kuwa, karibu asilimia 67 ya
Wamarekani wenye kipato cha chini wana wasiwasi mkubwa wa kukumbwa na
umaskini mkubwa zaidi na kupoteza makazi yao.
Uchunguzi huo unaonesha
kuweko ongezeko kubwa la Wamarekani wenye wasiwasi wa kukumbwa na
matatizo hayo ikilinganishwa na miaka ya 2010 na 2011.
Uchunguzi
wa huko nyuma wa maoni ulionesha kuwa asilimia 51 ya raia wa Marekani
walikuwa na wasiwasi wa kuongezeka umaskini na kupoteza makazi yao.
Utafiti
wa shirika la Gallup uliofanywa mwaka 2014 nchini Marekani ulionesha
kuwa idadi ya Wamarekani waliokuwa na wasiwasi wa kupoteza makazi yao na
kuongezeka umaskini wao haikupindukia asilimia 35 wakati huo.
Machafuko,
vitendo vya utumiaji mabavu, uhalifu, jinai na ukosefu wa amani na
usalama ni mambo mengine yanayozifanya nyoyo za wananchi wa Marekani
kuwa na wasiwasi mkubwa hususan kati ya matabaka ya watu maskini na
wenye kipato cha chini.
Matokeo
ya uchunguzi wa hivi sasa wa taasisi ya Gallup unaonesha kuwa
Wamarekani wa matabaka yote wana wasiwasi wa kupoteza makazi yao na
kuongezeka umaskini na kwamba idadi yao imeongezeka sana hivi sasa
ikilinganishwa na miaka ya huko nyuma
SHARE
No comments:
Post a Comment