Mama Salma Kikwete, mke wa Rais mstaafu
wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete, amekula kiapo cha uaminifu mbele
ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Aprili 4, 2017. Mama
Salma aliteuliwa hivim karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kuwa Mbunge katika nafasi 10 za Rais
za kuteua wabunge. Katika tukio lingine, mumewe, Dkt. Jakaya Kikwete,
amemshangaza Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, baada ya kushangiliwa kwa
nguvu na wabunge, pale alipomtambulisha mbele yao. "Katika vipindi
vyangu vinne kama mbunge sijawahi kuona mtu akishangiliwam namna hii".
Hayo yalikuwa maneno yaSpika Ndugai, ambaye baada ya kuona nderemo,
vifijo na bashasha zimezidi, alitoa rukhsa kwa wabunge kuonyesha
ushangiliaji wa "kujiachia" aliwaruhusu kusimama ili kuonyesha heshima
kwa kiongozihuyo mstaafu ambaye alifuatana na mmoja wa watoto wake wa
kiume Ally Kikwete. Pichani mama Salma akiwasili kwenye viwanja vya
bunge mjini Dodoma leo. (PICHA NA RAYMOND MUSHUMBUSI WA MAELEZO)
Mama Salma akisindikizwa na wabunge wanawake kuelekea mbeleya bunge kula kiapo
Mama Salma akila kiapo mbele ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai
Mhe. Job Ndugai akimtambulisha Rais Mstaafu Kikwete kwa wabunge
Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete,
9katikati), akiwa na mwanaye wa kiume Ally Kikwete, (kushoto) na
msaidizi wake, bungeni mjini Dodoma leo Aprili 4, 2017
Dkt. Kikwete, akiongozwa na Katibu Myeka wa Spika wa Bunge, Bw. Said Yakubu, (kushoto)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.
Angella Kairuki akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha
Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsi Wazee na Watoto Mhe.
Ummy Mwalimu akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha
Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda akisalimia
wabunge mara baada ya kutambulishwa kati ya wageni wa Spika leo Bungeni Mjini
Dodoma kushoto ni Mke wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mama Devotha Gabriel.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Ajira na
Watu wenye Ulemevu Mhe. Jenista Mhagama akitengua kifungu cha Bunge kwa kuomba
Bunge kuendesha shughuli zake siku ya Jumamosi na siku za kazi kuendelea kwa
awamu ya pili saa kumi jioni badala ya saa kumi na moja jioni.
SHARE
No comments:
Post a Comment