Julian
Msacky
KWA muda
mrefu sasa tunaridhia maazimio mbalimbali ya kimataifa, lakini utekelezaji wake
unakuwa wa kusuasua.
Tatizo
hili halipo tu hapa kwetu bali linahusu nchi karibu zote za dunia ya tatu na hivyo
kukwama kimaendeleo.
Wakati
tukisuasua kiutekelezaji Umoja wa Mataifa (UN) unaendelea kuchanja mbuga kwa
kuanzisha malengo mengine
Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres
Kwa mfano,
hivi sasa umoja huo umezindua Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Malengo
hayo yamepatikana baada ya
kumalizika
kwa Mpango wa Maendeleo ya Milenia (MDGs).
Hebu
tujiulize malengo yaliyokuwa katika mpango huo wa MDGs ulidumu kwa miaka 15 yalitimia
kama ilivyotakiwa?
Chini ya
MDGs tulitakiwa tuwe tumemaliza umaskini, lakini tatizo hilo linaendelea kwa kasi
kubwa na ufumbuzi wake ni bado.
Tunafahamu
kuwa umaskini ndiyo adui mkubwa wa maendeleo. Mwenye tatizo hilo hawezi kulima
inavyotakiwa.
Mwenye
umaskini hawezi kutunza afya yake inavyotakiwa na pia hana ubavu wa kufuta
ujinga kwani hana hili wala lile.
Maskini
hana habari za kutunza mazingira, mwenye umaskini hana uhakika wa kuwa na
makazi bora. Ni tatizo kweli kweli.
Kwa hiyo
tunapozungumzia malengo ya maendeleo endelevu ni lazima tuhakikishe watu
wanaondokana na umaskini.
Bila
kufanya hivyo tutaanzisha mipango lukuki bila mafanikio. Ushauri wangu ni
muhimu tuwe makini kuridhia maazimio.
Endapo
tumejiridhisha kuwa MDGs hatukufanya vizuri hatuna sababu ya kuridhia maazimio
mengine ya UN.
Nalisema
hili si kwa nchi yangu tu bali na mataifa mengi ya Afrika kwani tatizo lililopo
Tanzania lipo pia Msumbiji.
Ni heri
nchi zetu ziwe wazi kwa UN badala ya kuendelea kusonga mbele wakati maazimio ya
nyuma hayakufanyikiwa.
Nikiangalia
ni nchi ngapi za Afrika zimefanikiwa kumaliza tatizo la umaskini katika malengo
ya MDGs sioni.
Kutunza
mazingira na kupunguza vifo vya wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka
mitano bado lipo tu.
Ndiyo
maana Rais wa Chama cha Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya
akina Mama
na Uzazi Tanzani
Profesa
Andrea Pembe
anasema
takwimu zinaonesha
akina mama
556
kati ya
wajawazito 100,000
hufariki
wakati wa ujauzito
na
kujifungua kila mwaka.
Idadi hii
bado ni kubwa kama alivyokiri Waziri mwenye dhamana ya afya, Ummy Mwalimu hivi
karibuni.
“Kwa
bahati mbaya nchi
yetu bado,
ukiangalia takwimu
zilizotolewa
Desemba
mwaka
jana, bado tuna idadi
kubwa ya
vifo vya uzazi
kwani
takriban kila wanawake
100,000
wanaojifungua,
wanawake
556 hufariki,”anasema.
Kwa maana
hiyo elimu ya afya uzazi inahitajika kwa kiwango kikubwa ili kuokoa maisha ya mama
zetu.
Kama
anavyosema Prof Pembe kuwa,“ jamii kama itaelewa nyakati
za hatari
wakati wa ujauzito
na
kujifungua itakuwa rahisi
kuchukua
hatua mapema kwa
kwenda
kwenye kituo cha
afya na
kuepuka vifo,”.
Ifike
mahali tuondokane na vifo hivyo kwa kuhakikisha tunawekeza vya kutosha katika
masuala ya afya.
Tunapozungumzia
malengo ya maendeleo endelevu maana yake huduma za kijamii zinatakiwe ziwe bora
na uhakika.
Ndiyo
maana ya endelevu. Lakini haiwezi kuwa endelevu kama watu hawana uhakika wa maji
safi na salama.
Hawana
uhakika wa afya bora. Hana umeme wa uhakika na badala yake wanaparamia misitu
ili waweze kuishi.
Maendeleo
endelevu ni dhana pana na kwa sababu hiyo nchi yetu ni lazima isimame imara
kuangalia vipaumbe muhimu.
Ni wakati
muafaka kutilia mkazo elimu ya afya kuanzia shule za msingi. Muhimu hapa ni
kuvunja ukimya.
SHARE
No comments:
Post a Comment