TRA

TRA

Friday, April 28, 2017

Wa-Baha’i wa ulimwengu mzima wanasherehekea Sherehe ya Ridvan

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Sherehe Kuu Kabisa ya Baha’i, Sherehe ya Ridvan (Riz-wahn) maarufu kama Sherehe Kuu Kabisa na Mfalme wa Sherehe, itasherehekewa na Wa-Baha’i kote duniani kuanzia tarehe April 20, 2017 hadi Mei 1, 2017. 


Hii ni Sherehe Takatifu Kabisa inayoadhimisha kipindo ambamo Baha’u’llah, Mtume Mwanzilishi wa Imani ya Baha’i, alitangaza kuwa Yeye Alikuwa Yule Mwahidiwa wa dini zote zilizotangulia.

 Mnamo mwaka 1863, Yeye alitangaza kuwa Yeye ndiye alikuwa “Yule Ambaye Mungu angemdhihirisha” na Mdhihirishaji wa Mungu kwa siku hii.

Baha’u’llah na familia Yake walilazimishwa kuhama kutoka nchi Yake ya kuzaliwa, Iran. 


Alikuwa mfungwa chini ya ufalme wa Ottomani wa Uturuki kwa kipindi cha miaka arobaini kwa sababu Yeye alikuwa ametangaza dini mpya, Imani ya Bahá’í.  

Baha’u’llah alikuwa kifungoni Baghdad, Iraq kwa muda wa miaka kumi na moja ya kifungo Chake. Kabla ya kuhamishiwa kutoka Baghdad kwenda Konstantinopoli (Istanbul ya  leo,Uturuki), Baha’u’llah alipitisha siku kumi na mbili katika bustani moja karibu na Baghdad akikutana na wafuasi Wake.
 Yeye aliita bustani hiyo Bustani ya Ridvan, ambayo maana yake ni “Paradiso” au “furaha njema” katika lugha ya Kiarabu. Baha’u’llah anaziita  siku hizo kumi na mbili Ridvan, Shere Kuu Kabisa na Mfalme wa Sherehe.

Wafuasi wengi sana wa Baha’u’llah walimtambua Yeye kama Hakimu, Mleta sheria na Mkombozi wa wanadamu wote, kama Mleta utaratibu wa sayari nzima, Mwunganishi wa watoto wa watu, na Mzinduzi wa millennia iliyongojewa kwa muda mrefu, kama Mwanzilishi wa “Duru Jipya la Muumbo” Msitawishaji wa Amani Kuu Kabisa, kama Chemchemi ya Haki Kuu Kabisa,  ka Mtangazaji wa zama zinazokuja za mbari mzima wa watu, kama Muumba wa Utaratibu Mpya wa Ulimwengu na Mhamasishaji naa Mwanzilishi wa Ustaarabu wa ulimwengu mzima.

Baha’u’llah alifundisha: “Kwamba mataifa yote yakusanyike kuwa taifa moja katika imani na watu wote ni ndugu; kwamba mafundo ya upendo kati ya watoto wa watu utaongezeka kuwa wenye nguvu; kwamba tofauti za kidini sharti ziishe, kwamba tofauti za kimbari zifutiliwe mbali—ugomvi huu usiokuwa na faida, vita hivi viharibifu vitaishilia mbali, na Amani Kuu Kabisa itakuja….Mapigano haya na umwagaji huu wa damu lazima viishe, na watu wote watakuwa ndugu moja na familia moja…Mwache mtu asijivunie hili kwamba analipenda taifa lake; bali  ajivunie hili kwamba anawapenda watu wenzake… Dunia ni nchi moja na wanadamu ni raia wake”.

Katika kipindi cha Ridvan, Wa-Baha'i kila mwaka  huwachagua wajumbe wa vyombo vyao vya kiutawala vya mahali na kitaifa, ambavyo vinajulikana kama Mabaraza ya Kiroho. Baha'u'llah alifundisha kuwa katika zama hizi za elimu ya wote, hakuna ulazima wa kundi maalum la watu kama makasisi. Badala yake, Alitoa mfumo wa kazi kwa ajili ya kusimamia  masuala ya Imani kupitia utaratibu  wa mabaraza yaliyochaguliwa kwenye ngazi za mahali, kitaifa, na kimataifa. Uchaguzi wa Ki-Baha'i hufanyima kwa kura ya siri na kura ya wengi, bila wagombea, uteuzi ama kampeni.

Jumuiya ya Bahá’í ya Tanzania inajiunga na Wa-Baha’i zaidi ya milioni sita ulimwenguni kote ambao wanaishi katika zaid ya maeneo 120,000, kwa ajili ya kusherehekea Sherehe ya Ridvan kutoka Alhamisi, tarehe 20 April, 2017 hadi Jumatatu, tarehe 1 Mei, 2017.

Jumuiya ya Ki-Baha’i ya Dar es Salaam itaadhimisha sherehe ya siku ya kumi na mbili ya Ridvan, siku ya Jumatatu, tarehe 1 Mei, 2017 saa 10:00 jioni katika Baha’i Senta,mtaa wa Mfaume Road, Upanga Magharibi. Ratiba itakuwa na sehemu ya ibada  ambamo sala na dua za Ki-Baha’i zitasomwa;  burudani  ya nyimbo, maongezi na chakula vitafuata. Kila mtu anakaribishwa sana kujiunga nasi kusherehekea Sherehe  hii Takatifu Kabisa ya Ridvan.kuja kwenu ndio mafanikio ya sherehe. 

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger