Waziri Mkuu wa Serbia Aleksandar Vucic ameibuka mshindi katika
uchaguzi wa rais. Vucic ameahidi kuendeleza jitihada za kujiunga na
Umoja wa Ulaya, lakini pia kuendeleza mahusiano na Urusi pamoja na
China.
Matokeo hayo ni pigo kwa upinzani uliorudi nyuma na kugawanyika. Vucic alishinda zaidi ya asilimia 55 ya kura zote zilizopigwa, kulingana na makadirio ya Kituo Huru cha Chaguzi za Kidemokrasia (CeSID).
Rais aliyepo madarakani Tomislav Nikolic, ambaye ni muasisi wa chama cha SNS kinachoongozwa sasa na Vucic, alishinikizwa na waziri mkuu huyo na kuamua kutogombea muhula mwingine wa miaka mitano.
Vucic alisema Jumapili, kwamba atabaki kama waziri mkuu kwa miezi miwili ijayo. Muhula wa urais Nikolic utamalizika Mei 31.

No comments:
Post a Comment