Rais wa Marekani, Donald Trump amesema Marekani ipo tayari
kulishughulikia suala la kitisho cha silaha za nyuklia cha Korea
Kaskazini iwapo China peke yake itashindwa kuchukua hatua.
Trump na Rais wa China Xi Jinping wanatarajiwa kukutana kwa mara ya kwanza baadaye wiki hii katika jimbo la Florida.
Viongozi hao wawili wanatarajiwa kujadili mvutano unaoendelea kuhusu Bahari ya Kusini ya China na kitisho cha mpango wa nyuklia cha Korea Kaskazini.
Marekani imekuwa ikiishinikiza China kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya Korea Kaskazini.
Katika mahojiano na gazeti la masuala ya biashara linalochapishwa Uingereza la Financial Times, Trump amesema iwapo China haitotoa ushirikiano wake, basi Marekani itachukua hatua peke yake.

No comments:
Post a Comment