TRA

TRA

Monday, May 22, 2017

Hofu yatanda minyoo kwenye nyama ya ng’ombe, nguruwe

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Mamlaka ya Dawa na Chakula Tanzania (TFDA) imesema kwamba taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii  kuhusu vijidudu vyeupe katika nyama ya ng’ombe ni ya ukweli, lakini akataka watoaji taarifa kama hizo waiarifu wizara kwanza.

Wataalamu wanakielezea kijidudu hicho kuwa ni mnyoo ambao unaweza kusababisha binadamu akapata kifafa, kukonda, kupata kichefuchefu, kupoteza hamu ya kula, maumivu ya tumbo na kuwashwa sehemu ya haja kubwa.

                                       Nyama
 
Hivi karibuni, taarifa hiyo ilisambaa katika mitandao ya kijamii na makundi ya WhatsApp ikiwatahadharisha wananchi kutokula nyama ya ngo’mbe yenye vijidudu vyeupe.

Taarifa hiyo, iliambatana na picha ya nyama iliyozungushiwa duara sehemu yenye alama nyeupe kuonyesha kuwa nyama ya aina hiyo ina kijidudu hicho.
Taarifa hiyo inasema kijidudu hicho kinaitwa Cystcercusbovis ambacho huingia mwilini mwa ng’ombe anapokula majani yenye kinyesi na huingia kwa binadamu anapokula nyama ya ng’ombe huyo isiyoandaliwa vizuri.
Pia, taarifa hiyo inasisitiza kuwa ng’ombe akiwa na wadudu hao hafai kuliwa na anatakiwa kufukiwa.
Msemaji wa TFDA, Gaudensia Simwanza aliliambia gazeti hili kwa simu jana kuwa ni kweli taarifa hiyo lakini hasa hawajui nani aliyeitoa kwa umma.
“Inawezekana ni mtaalamu, tunamshukuru kwa kuujulisha umma. Lakini nitoe wito kwa Watanzania kama wana taarifa za kitaalamu kuhusu vyakula ni vyema wakawasiliana moja kwa moja na TFDA,” alisema Gaudensia.
“Ndiyo maana katika machinjio ya mifugo tunaweka madaktari na nyama ikibainika ina matatizo inateketezwa,” alisema Gaudensia.
Wataalamu wanakielezea kijidudu hicho kuwa ni mnyoo ulio katika hatua ya awali.
“Kwa jina jingine unaweza kuita lava,” alisema Dk Rickey Fidelys.
Alisema vijidudu hivyo vipo aina tatu, lakini Dk Fidelys alizitaja aina mbili ambazo ni Taenia Sollium au T. Sollium anayepatikana kwenye nyama nguruwe na Taenia Saginata au T. Saginata kwenye nyama ya ng’ombe.
“T. Saginata hana madhara makubwa kwa binadamu tofauti na TSollium. Minyoo hii hukua katika mwili wa binadamu na ndiyo hatua ya mwisho ya ukuaji wao,” alisema Dk Fidelys.
Alisema T. Sollium humuingi a ng’ombe utumboni na  kisha kusambaa maeneo mengine.

CHANZO: MWANANCHI

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger