Baada
ya usiku wa May 10 kufahamu fainali ya UEFA Champions League
itazikutanisha timu gani, usiku wa May 11 2017 ndio ilichezwa michezo ya
marudiano ya nusu fainali ya UEFA Europa League, Man United wakicheza
dhidi ya Celta Vigo na Lyon wakicheza dhidi ya Ajax.
Game
ya Man United ilimalizika kwa sare ya kufungana 1-1 goli la Man United
likifungwa na Fellaini dakika ya 17 na goli la Celta Vigo lilifungwa
dakika ya 85 na Roncaglio, sare hiyo imeiwezesha Man United kuingia
hatua ya fainali baada ya mchezo wa kwanza kuifunga Celta Vigo goli 1-0
ugenini.
Ajax
wao wamepoteza kwa magoli 3-1 lakini wamefuzu kuingia fainali kwa
aggregate ya 4-5, Man United anafuzu kucheza fainali ya Europa League
kwa mara ya kwanza wakati Ajax anafuzu kucheza fainali hizo kwa mara ya
kwanza baada ya miaka 21 mara ya mwisho ilikuwa 1996.
Mchezo
wa fainali ya UEFA Europa League itachezwa katika uwanja wa Friends
mjini Stockholm nchini Sweden May 23 2017, hii inakuwa ni mara ya pili
kwa kocha wa Man United Jose Mourinho kufanikiwa kufikia hatua ya
fainali ya michuano hiyo akiwa na timu mpya katika msimu wa kwanza, mara
ya kwanza ilikuwa 2002/03 akiwa na FC Porto ya kwao Ureno.
SHARE
No comments:
Post a Comment