Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu
(aliyevaa Kaunda suti) akiwasili katika Viwanja vya Kyaikarabwa kutembelea na
kukagua shughuli zinazoendelea wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa inayofanyika
kitaifa mkoani Kagera.
Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu
akimsikiliza Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TABD, Bw. Saidi Mkabakuli wakati
alipotembelea Banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwenye
Viwanja vya Kyaikarabwa yanapofanyika Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa mkoani
Kagera.
Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu
akikaribishwa katika Banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na
Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TABD, Bw. Saidi Mkabakuli.
Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu
(aliyeshika kipaza sauti kulia) akizungumza wakati alipotembelea Banda la TADB.
Anayemsikiliza kushoto ni Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TABD, Bw. Saidi
Mkabakuli.
Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TABD, Bw. Saidi Mkabakuli
akisisitiza jambo wakati Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu) Salum
Kijuu (hayupo pichani) alipotembelea Banda la TADB.
|
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukoba, Bibi Mwantum Dau (kulia)
akifurahia jambo na na Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TABD, Bw.
Saidi Mkabakuli wakati wakimsubiri Mkuu wa mkoa wa Kagera.
Na mwandishi wetu, Bukoba
Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu
amewaasa wakulima na wafugaji wa mkoa wa Kagera kuchangamkia fursa za mikopo
inayotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kujikwamua
katika shughuli zao za kilimo mkoani humo.
Meja Jenerali (Mstaafu) Kijuu alitoa wito huo alipotembelea Banda
la TADB wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa inayofanyika kitaifa mkoani
Kagera.
Mkuu wa mkoa huyo alisema kwa kuzingatia malengo ya uanzishwaji wa
Benki ya Kilimo unalenga kutimiza dhamira ya Serikali ya kuwasaidia wakulima
nchini kote kukabiliana na mapungufu kwenye kuongeza tija katika shughuli zao
za kilimo.
“Nawaomba wakulima na wafugaji wa Kagera kuchangamkia mikopo nafuu
ya Benki yetu ya Kilimo ili muongeze tija katika kilimo chenu maana Benki ipo
kwa ajili ya kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza
mapinduzi katika kilimo nchini,” Meja Jenerali (Mstaafu) Kijuu
alisihi.
Kwa mujibu wa TADB, sekta za kilimo na mifugo ni sekta za
kipaumbele ambazo zinazopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao
na mifugo hasa katika uongezaji wa thamani wa sekta hizo nchini.
Benki hiyo inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya Muda
Mfupi (Hadi Miaka Miwili (2)), Mikopo ya Muda wa Kati (Zaidi ya Miaka 2 hadi
Miaka Mitano (5)) na Mikopo ya Muda Mrefu (Zaidi ya Miaka 5 hadi Miaka Kumi na
Mitano (15)).
TADB ni taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya
kutatua ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya
kilimo nchini ambao ulikuwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi
kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa;
riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya
kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo na mazao
ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
SHARE
No comments:
Post a Comment