Mfuko wa Pensheni wa PPF
umeendelea kukabidhi vifaa tiba katika hospitali na vituo vya afya
nchini kulingana na sera yake ya uchangiaji na udhamini. Katika wilaya
ya Kisarawe, Mfuko wa PPF umekabidhi vifaa tiba hivyo kwa Naibu Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI,Utumishi na Utawala bora Mhe. Selemani
Jaffo kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambavyo ni vitanda 2
vya kujifungulia wakinamama, vitanda 4 vya wagonjwa wa kawaida, mashuka
56 na vifaa vinavyotumika kujifungulia wakinamama.
Akipokea vifaa hivyo, Mhe. Jaffo
alisema Mfuko wa PPF walichofanya ni jambo kubwa kwa vile hospitali za
wilaya ya Kisarawe zilikuwa zikikabiliwa na changamoto katika sekta ya
afya.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano
wa PPF, Lulu Mengele, alisema Mfuko umetoa vifaa tiba hivyo ikiwa ni
muendelezo wa zoezi la kurudisha kwenye jamii kulingana na sera ya
uchangiaji na udhamini ya PPF. Alisema Kisarawe ni wilaya ya nne kupata
vifaa hivyo na kwamba wataendelea kutoa kwenye hospitali nyingine 12
nchini. Lulu alisema Mfuko wa PPF, umetoa vifaa tiba vyenye jumla
thamani ya Sh. 99,983,700/-.
Shughuli hiyo ya kukabidhi vifaa
tiba kutoka Mfuko wa PPF ilienda sambasamba na taarifa ya kukabidhi
vifaa tiba kutoka kwa Mfamasia Mfawadhi wa Ofisi ya Rais
(TAMISEMI),Regina Joseph kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
TAMISEMI, Utumishi na Utawala bora Mhe. Selemani Jafo, alisema kuwa Rais
Dkt. Magufuli ametoa vitanda 20 vya kulalia, vitanda sita vya
kujifunguli. Vifaa kama hivyo vinasambazwa katika hospitali nyingine
nchi nzima.
Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala
Bora, Seleman Jaffo akiongea na wafanyakazi na wananchi waliojitokeza
katika halfa ya kupokea vifaa tiba ikiwemo vitanda 2 vya kujifungulia
wakinamama, vitanda 4 vya wagonjwa wa kawaida, mashuka 56 na vifaa
vinavyotumika kujifungulia wakinamama kutoka kwa Mfuko wa PPF katika
kutekeleza sera yake ya uchangiaji na udhamini. PICHA ZOTE NA CATHBERT
KAJUNA WA KAJUNASON BLOG-KISARAWE.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Nedesa akielezea machache
juu ya changamoto zilizokuwa zikiikabili wilaya yake katika upande wa
afya. Pembeni yake ni Naibu wa Waziri (TAMISEMI), Utumishi na Utawala
Bora, Seleman Jaffo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe, Hamis
Dikupatile.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Lulu Mengele akiongea wakati
wa halfa ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika jana katika hospitali ya
Wilaya ya Kisarawe, Pwani.
Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Seleman Jaffo akipokea
msaada wa vifaa tiba kutoka Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Lulu
Mengele wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa tiba iliyofanyika jana katika
hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani.
Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoaa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala
Bora, Seleman Jaffo akimkabidhi vifaa tiba kwa Mganga mkuu wa Wilaya ya
Kisarawe, Elizabeth Oming’o kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya
Kisarawe.
Vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko wa PPF.
Naibu wa Waziri wa Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoaa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala
Bora, Seleman Jaffo (wa tano toka kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,
Happyness Nedesa wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya wafanyakazi wa
Mfuko wa PPF na wafanyakazi wa wilaya ya Kisarawe.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe, Hamis Dikupatile akitoa shukrani Mfuko wa PPF kwa kutoa vifaa tiba.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF, Janet Ezekiel (wa pili
kulia) na Afisa Uendeshaji wa PPF Kanda ya Ilala, Stella Mashiku
wakiwaandikisha mwanachama mpya wa Wilaya ya Kisarawe, Pwani.
Afisa Uendeshaji wa PPF Kanda ya Ilala, Stella Mashiku akiwaandikisha wanachama wapya wa Wilaya ya Kisarawe, Pwani.
SHARE
No comments:
Post a Comment