NA K-VIS BLOG, RUKWA
KATIKA kuhakikisha Mkoa wa Rukwa Upo salama kutokana
na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola yatakayoweza kujitokeza, Mkuu wa Mkoa
wa Rukwa Kamishna (Mstaafu) Zelote Stephen(pichani) amefanya ziara ya siku tatu
katika mwambao wa ziwa Tanyangika kwenye Kata ya Kirando, Kabwe na Kasanga
vijiji ambavyo vipo jirani na nchi ya DRC ili kujionea namna Halmashauri
ya Nkasi na Kalambo zilivyojipanga kuhakikisha kuwa ugonjwa huo hautii mguu
katika Mkoa na nchi kwa ujumla.
Ziara hiyo aliianza siku ya Ijumaa tarehe 26 hadi 28.
05. 2017 mara baada ya kumaliza kumalizika kwa mafunzo ya siku tatu yaliyohusu
utumaji wa taarifa za magonjwa kwa kieletroniki (e-idsr) yenye kusisitiza
tahadhari ya ugonjwa wa ebola uliopo katika nchi jirani ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yaliyotolewa kwa wahudumu wa afya wa Serikali na
Sekta binafsi kwa Halmashauri mbili za Manispaa ya Sumbawanga na Sumbawanga vijijini.
Mafunzo ya awamu ya pili yanatarajiwa kumalizika
tarehe 31. 05. 2017 kwa Halmashauri za Kalambo na Nkasi ikiwa ni muendelezo wa
awamu ya kwanza kwa Halmashauri ya Sumbawanga Vijijini na Manispaa ya
Sumbawanga yaliyoisha tarehe 26. Mwezi wa tano.
Ili kujiridhisha na maandalizi ya Halmashauri
zinazopakana na nchi za jirani yaani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
pamoja na Zambia Mkuu wa Mkoa alipita katika bandari maarufu za pwani ya ziwa
Tanganyika na kuongea na vyombo vya usalama ikiwemo uhamiaji, Sumatra, TRA,
jeshi la polisi, jeshi la wananchi, maafisa forodha pamoja na maafisa afya
kutoka Wilayani.
Pia Mh. Zelote aliongea na viongozi wa serikali za
vijiji na kata wakiwemo madiwani, watendaji wa kata na vijiji, wenyeviti wa
vijiji na vitongoji, maafisa ugani wa kata na vijiji, maafisa afya wa kata na
vijiji na kufanya mikutano ya hadhara ili kuwapa wananchi ujumbe aliokwenda nao
katika kuhakikisha ugonjwa huo haunusi katika mkoa wa Rukwa na nchi ya
Tanzania.
Pamoja nae Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa aliambatana na
Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface Kasululu, Mratibu wa Chanjo Mkoa Gwakisa
Pamoja na Afisa kutoka Wizara ya Afya wa usimamizi na ufuatiliaji Solomon
Mushi, Mkuu wa Wilaya, makatibu tawala wa wilaya pamoja na kamati za ulinzi na
usalama za Wilaya.
Katika kila Wilaya aliyopita Mh. Zelote alihakikisha
anapewa taarifa za maandalizi ya Wilaya na kisha kwenda kwenye mipaka ili
kujionea kwa macho yake maandalizi hayo na pia kuongea na wananchi wanoishi
karibu na mipaka hiyo.
Wakati akiwa kwenye ziara hiyo Mh. Zelote alikuwa
akisisitiza utayari pamoja na kujihadhari kwa viongozi wa serikali za vijiji na
kata na pia kwa vyombo vya usalama vya maeneo hayo ya mipakani.
Katika suala la utayari Mh. Zelote Alisema kuwa
wananchi wanapaswa kuelimishwa juu ya athari ya ugonjwa huo na namna ya
kujikinga nao ikiwa ni pamoja na kuelezwa dalili za ugonjwa na njia za
maambukizi ya ugonjwa huo na kuwasisitiza wananchi kwenda zahanati pindi
wanapojiskia kuumwa na sio kukimbilia kwenye maduka ya dawa na kuagiza vidonge
bila ya kujua ugonjwa anaoutibu.
Pia katika kusisitiza hilo Mh. Zelote aliwasihi
wananchi kutokimbilia kwa waganga wa kienyeji pindi wanapoumwa na badala yake
wakimbilie kwa wataalamu wa afya kwenye zahanati ama vituo vya afya. Na
kuwaonya kuwa kupitia hizi taarifa za ugonjwa wa ebola kunaweza kukajitokeza
matapeli ambao watajitangaza kuutibu ugonjwa huo jambo ambalo si kweli, hivyo
aliweka msisitizo kuwa ugonjwa wa Ebola hauna Tiba.
“Mtu yeyote atakayejiskia vibaya basi haraka akimbilie
kwenye zahanati ama kituo cha afya na sio kwa mganga wa kienyeji, na mjiepushe
mbali sana na matapeli wanaotibu watu vichochoroni ama wanaosema dawa ya
Ebola ipo,…. Hakuna,” Mh. Zelote alieleza.
Pamoja na hayo Mh. Zelote alionya kuwa katika
kusimamia jambo hilo hatakuwa na utani, dhihaka ama masihara kwayeyote
atakaekiuka taratibu zilizowekwa ili kujihadhari na ugonjwa huo kuingia katika
mkoa wa Rukwa.
“Mimi nafahamu
kwamba watu wanaoishi humu kwenye mipaka wameoa ama kuolewa katika nchi za
jirani, na kwamba watanzania utamaduni wetu ni ukarimu kwa wageni lakini katika
hili tupunguze ukarimu mpaka jambo hili liishe, na yeyote atakayegundulika
anamhifadhi mgeni kinyume na taratibu, huyo ni mhalifu,” Mkuu w Mkoa alisema.
Katika kuonesha athari kubwa inayoweza kupatikana
endapo uginjwa huo utapenya katika nchi yetu Mh. Zelote alieleza kuwa gharama
za kumshughulikia mgonjwa mmoja ni kubwa sana na kuongeza kuwa endapo ugonjwa
huo unathibitishwa kwenye nchi Fulani basi tatizo hilo si la nchi hiyo tu ni la
dunia nzima.
“Nguo inayotumika kumshughulikia mtu mmoja inauzwa
milioni 10 na kwa wenzetu huko afrika ya magharibi Ivory Coast ambako
walikumbana nao watu 11,000 walifariki, wakiwemo madaktari ambao walikuwa
wakiwauguza wagonjwa, mtu mmoja tu akiupata basi kijiji kizima kinafungwa
hakuna mtu kuingia katika kijiji hicho wala kutoka,” Mh. Zelote alisisitiza.
Lakini pia aliwatoa hofu wananchi na kuwaambia kuwa
mpaka sasa Tanzania hakuna mgonjwa hata mmoja wa Ebola.
Nae Daktari wa Mkoa Dkt. Kasululu alisema kuwa tangu
ugonjwa huo kutolewa taarifa na Wizara ya Afya tarehe 12. 05. 2017 watu watatu
wlikuwa wamefariki na wengine 12 walikuwa wako chini ya uangalizi lakini hadi
kufuikia tarehe 25. 05. 2017 idadi ya wagonjwa iliongezeka hadi kufikia
wagonjwa 45 na kuongeza kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka kadiri siku
zinavyokwenda mbele.
“Idadi ya
wagonjwa imekuwa ikiongezeak kila kukicha hivyo ni jukumu letu kuhakikisha
tunajiandaa na kujihadhari kweli, maana wagonjwa hawa wapo kwenye misitu ambapo
usafiri wa kawaida haufiki isipokuwa Helkopta na pikipiki, hivyo wagonjwa
wanaweza kuwa wengi na bado hawajajulikana,” Dkt Kasululu alisisiza.
Nae Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Dk. Makundi
Maige alielezea mikakakti ya Halmashauri ya Nkasi namna ilivyojipaga
kuhakikisha wanakaa mbali na ugonjwa hatari wa Ebola.
“ Wilaya imeainisha kata tatu za Kirando, Kabwe na
Wampembe ambazo zimetengwa kwaajili ya kupokea wageni kutoka nchi za jirani,
tukifahamu kuwa katika mwambao wa Ziwa Tanganyia kuna Kata 10 ambazo ugonjwa
huu unaweza kuingia kwa urahisi, ambazo ni Kabwe, Kirando, Wampembe, Itete,
Kipili, Mkinga, Korongwe, Ninde, Kizumbi na Kala,” Dk. Makundi aliainisha.
Katika kubainisha upokezi wa wageni hao Dk. Makundi
alisema kuwa kituo cha Wampembe kitapokea wageni wanoelekea kijiji cha Kilambo
hadi Msamba, Kituo cha Kirando kitapokea wageni wanaoelekea kijiji cha Ninde
hadi Kazovu na kituo cha Kabwe kitapokea wageni wanaoelekea kijiji cha Utinta
hadi Kalila.
Na kuongeza kuwa wageni wote kutoka nchi za jirani
watalazimika kupitia katika vituo hivyo na sio kuingia kiholela kama
ilivyozoeleka na kabla ya kuendelea na safari zao watakuwa wakichunguzwa afya
zao.
Kwa kuzingatia namna ugonjwa huo unavyoenea Wilaya
imetenga eneo maalum kwaajili ya matibabu ili kuepuka kuchanganya wagonjwa
watakaobainika kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola.
Pamoja na hayo Wilaya imejipaga kuzizungukia kata zote
10 na kutoa elimu kwa wananchi na viongozi wa maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na
kuwashirikisha viongozi wa dini, wazee maarufu, vijana, waalimu na wanafunzi
juu ya ugonjwa huo hatari.
Nao upande wa Wilaya ya Kalambo walieleza
mipango yao juu ya udhubiti wa ugonjwa huu, ambapo mganga Mkuu wa Wilaya Dkt.
Alcado mwamba aliweza uainisha tahadhari mbalimbali ambazo Wilaya imezichukua
kuhakikisha wanaudhibiti ugonjwa huo kutokuingia katika Wilaya hiyo.
Miongoni mwa tahadhari walizochukua ikiwa ni
kuwasambazia wananchi vipeperushi vyenye kutoa elimu ya ugonjwa wa Ebola lakini
pia kuihamasisha jamii kutoa taarifa haraka kwa uongozi wa serikali pindi tu
wakibaini kuna mgeni aliyeingia kinyume na taratibu zilizowekwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment