Meneja
wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, kulia akimkabidhi nyaraka
halali za Benki ya NMB zinazoonyesha kuingizwa kwa fedha za mshindi wao
Sospeter Muchunguzi pichani kushoto jumla ya Sh Milioni 10 alizoshinda
katika Bahati Nasibu yao ya Ijue Nguvu ya Buku, droo iliyochezeshwa
Jumapili. Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI
wa droo ya saba ya Sh Milioni 10 kutoka kwenye Bahati Nasibu ya Biko
'Ijue Nguvu ya Buku', Sospeter Muchunguzi, amekabidhiwa fedha zake huku
akisema kuwa kuogopa kucheza Biko ni dalili ya kukaribisha umasikini.
Muchunguzi
aliyasema hayo jana katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam wakati
anakabidhiwa fedha zake na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace
Kaijage.
Akizungumza
kwa msisitizo mkubwa, Muchunguzi mwenye ndoto za ujasiriamali alisema
kwamba watu wote waliofanikiwa katika maisha yao walithubutu katika
mambo waliyokusudia kuyafanya, hivyo ni budi kila mmoja kupita njia
hiyo.
Sospeter
Muchunguzi katikati akisaini nyaraka za benki ya NMB kwa ajili ya fedha
zake kuingizwa kwenye akaunti yake katika benki hiyo jana baada ya
kuibuka kidedea katika droo ya Biko ya Sh Milioni 10. Kulia ni Meneja wa
Huduma kwa Wateja wa Biko Grace Kaijage na kushoto ni Afisa wa NMB.
Alisema
uhakika wa kushinda ni mkubwa ikiwa mtu ameamua kweli kuingia katika
sekta ya michezo ya kubahatisha, hususan mchezo wa Biko ambao hata
uchezaji wake upo wazi na hakuna dalili zozote za kudanganya washindi.
“Nilipoona
utaratibu wa Biko ni mzuri nikathubutu kucheza huku nikiamini kwamba
endapo naweza kuibuka na ushindi naweza kusogea katika hatua moja kwenda
nyingine hivyo Watanzania wenzangu hakuna haja ya kuogopa ili tusonge
mbele.
“Nimefurahi
kupata fedha hizi kutoka Biko maana hata uchezaji wao kwa njia ya
ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo,
Vodacom na Airtel kwa kuandika kuingiza namba ya kampuni ambayo ni
505050 na kumbukumbu namba ya 2456 ni rahisi hali inayoweza kumfanya
kila mtu amudu kucheza mahala popote na wakati wowote,” Alisema
Muchunguzi.
Naye
Grace Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, aliwataka Watanzania kila
pembe za nchi kucheza kwa wingi ili wajiwekee mazingira ya kushinda
zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000,
100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazotoka kila wakati, huku pia
donge nono la Sh Milioni 10 likitolewa katika droo ya Jumatano na
Jumapili.
“Lengo
letu ni kutoa zawadi nono kwa kila mshindi wetu, hivyo umnachotakiwa
kufanya ni kucheza Biko kwa wingi kwa kununua tiketi kuanzia Sh 1000 na
kuendelea ili mshinde, maana kucheza mara nyingi zaidi ndio njia ya
kufanikisha ushindi,” Alisema Grace na kuongeza kuwa tiketi moja inatoa
nafasi mbili, ikiwamo ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na nafasi ya
kuingia kwenye droo ya kuwania Sh Milioni 10.
Kwa
mujibu wa Grace, washindi wao wanaoshinda zawadi za papo kwa hapo
wanatumiwa fedha zao kwa kupitia simu walizocheza na wale wa droo kubwa
wakikabidhiwa katika benki ili kuleta usalama wa fedha wanazotoa kwa
washindi wao.
SHARE
No comments:
Post a Comment