Kampuni
ya vinywaji baridi ya Coca-Cola hapa nchini, kwa ushirikiano na
TAMISEMI, imefanya uzinduzi wa mashindano ya umoja wa shule za sekondari
(Umisseta) kwa kanda ya Kaskazini, mkoani Arusha kwa kugawa vifaa vya
michezo kwa shule mbalimbali za sekondari za serikali na binafsi. Katika
uzinduzi wa mashindano hayo jijini Arusha, kwenye uwanja wa Sheikh Amri
Abeid mwishoni mwa wiki, mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mkuu wa
mkoa wa Arusha - Mrisho Gambo, ambapo aliishukuru kampuni ya Coca cola
kwa udhamini kufanikisha michuano yam waka huu. Kwa upande wake, Meneja
Mauzo wa Coca-Cola mkoa wa Arusha, Boniface Mwasi alisema kuwa kampuni
hiyo imeona umuhimu wa kuibua vipaji vya michezo ndio maana wamejikita
kufadhili michezo kama hiyo kwa vijana.
“Tumeamua
kushirikiana na serikali katika michezo hii ya Umisseta lengo letu
kubwa likiwa ni kuibua vipaji vingi vya michezo kwa kuwa tunaamini
mtandao wa shule za sekondari ni mkubwa na ni rahisi kuibua vipaji vingi
kutoka sehemu zote za nchi”, Alisema Mwasi. Aidha, aliongeza ya kwamba
kampuni ya Coca-Cola itaendelea kuunga mkono jitihaa za serikali za
kukuza sekta ya michezo nchini hususani katika ngazi za chini ambako
imekuwa ni vigumu kupata ufadhili kwa kuwa tunaamini kuwa vipaji
vinapaswa kuibuliwa na kukuzwa. “Tunayo dhamira kuona vijana wa
kitanzania walioibukia kwenye mashindano haya wanafika mbali kimichezo”,
Alisisitiza Mwasi.
SHARE








No comments:
Post a Comment