Wanajeshi wawili wamepoteza maisha baada ya kutokea
mripuko wa bomu la kutegwa ndani ya gari walipokuwa wakijaribu kulitegua
bomu hilo katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, hii leo.
Kwa mujibu wa afisa wa poolisi Meja Nur Ahmed aliyezungumza na
shirika la habari la Reuters, wanajeshi hao waliuwawa walipokuwa
wakivunja sehemu ya gari na kisha bomu hilo kuripuka.
Hakuna kundi lililodai mara moja kuhusika, ingawa wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab wameanzisha msururu wa mashambulizi mjini Mogadishu na maeneo mengine nje ya mji huo wakijaribu kulazimisha kuweka utaratibu wa sheria za Kiislamu.
Somalia iko katika vita tangu mwaka 1991 baada ya wababe wa kivita kumuangusha madarakani dikteta Siad Barre na baaday kugeukiana wenyewe kwa wenyewe.
CHANZO: DW

SHARE
No comments:
Post a Comment