TRA

TRA

Wednesday, May 31, 2017

Taifa Stars yaanza kambi nchini Misri

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Timu ya mpira wa miguu ya Tanzania inatarajiwa kuanza mazoezi yake usiku huu baada ya kufika salama mjini Alexandria,nchi Misri kwa ajili ya kuweka kambi.

Akizungumza mara baada ya kukagua viwanja vya mazoezi leo asubuhi, Kocha Mayanga ambaye alipewa majukumu ya kuifundisha timu hiyo mapema - Januari, mwaka huu, amesema: 

"Programu ya mazoezi kwa timu hii itaanza leo saa 2.00 usiku. Ingawa siku nyingine nitafanya asubuhi na jioni."

 Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga upande wa kulia akiwa na wasaidizi wake wakikagua Uwanja ambao utautumia kwa ajili ya mazoezi kwenye kambi ya Tolip Sports City, Alexandia, Misri.

Taifa Stars inayopiga kambi hapa Misri, inajiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho utakaofanyika Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Mchezo huo umepangwa kuanza saa 2.00 usiku.

Mchezo dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi 'L' kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika NCHINI Cameroon.
Mbali ya Lesotho na Tanzania, mataifa mengine katika Kundi 'L' ni Uganda na Cape Verde ambao pia wikiendi ya Juni 9, 10 na 11, mwaka huu watakuwa katika mchezo wa kwanza pia kuwania nafasi hiyo.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger