Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
ndani ya nchi, Mhe.Hamad Masauni akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini IGP Ernest Mangu wakati anawasili katika ukumbi wa mikutano wa
AICC kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la
Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO). Kulia ni
Mkuu wa INTERPOL kanda ya Kusini Mubita Nawa.( Picha na Hassan
Mndeme-Jeshi la Polisi)
Katibu Mtendaji wa SADC,
Dk.Stegnomena Tax akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP
Ernest Mangu kabla ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la
Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) unaofanyika
mkoani Arusha. IGP Mangu ndiye Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa kipindi
hiki. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi)
Baadhi ya Wakuu wa majeshi ya
Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika SADC wakitoa heshima wakati
wimbo wa taifa unapigwa wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa
mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika
(SARPCCO) uliofanyika Mkoani Arusha. IGP wa Tanzania, Ernest Mangu ndiye
Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa kipindi hiki. Picha na Hassan
Mndeme-Jeshi la Polisi)
Katibu Mtendaji wa SADC,
Dk.Stegnomena Taxi, akitoa hotuba wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano
mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini
mwa Afrika (SARPCCO) Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Waziri wa Wizara
ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe.Hamad Masauni Mkoani Arusha. IGP wa
Tanzania Mangu ndiye Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa kipindi hiki.
Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi)
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
ndani ya nchi, Mhe.Hamad Masauni akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu
wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa afrika (SARPCCO) baada ya ufunguzi
wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za
kusini mwa Afrika unaofanyika Mkoani Arusha. Picha na Hassan
Mndeme-Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,
IGP Ernest Mangu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
akiwa ameambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Angola, Paulo de Almeida
(kushoto) na Mkuu wa jeshi la Polisi la Msumbiji, Paulo Chachine
(kulia) wakati wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi
kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) uliofanyika Mkoani
Arusha.(Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
SHARE
No comments:
Post a Comment