BENKI ya NMB imezindua akaunti
mpya kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ijulikanayo kama ‘NMB
FANIKIWA ACCOUNT’ ili waweze kukua kibiashara pamoja na kupata maendeleo
ya biashara wanazozifanya.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa akaunti hiyo ya
wafanyabiashara wadogo na wakati, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo,
Ineke Bussemaker, alisema kuwa akaunti hiyo haina masharti magumu wakati
wa kuifungua pamoja na uendeshaji wake hivyo kuwataka wafanyabiashara
wote kuitumia.
Alisema kuwa NMB imebuni akaunti
hiyo kutokana na kuwepo kwa changamoto ya wafanyabiashara wadogo kukosa
mikopo na kukabiliwa na riba kubwa kwenye mikopo. Akifafanua zaidi juu
ya bidhaa hiyo, Mkuu wa Idara ya Biashara, James Meitaron alisema Benki
ya NMB imeweza kufikia kila kundi katika kuwanufaisha wafanyabiashara
wadogo hasa kimikopo ambapo imewanufaisha katika kuendeleza biashara
zao.
Alisema Benki ya NMB imekuwa
ikifanya kazi kwa ukaribu na serikali pamoja na taasisi zake, ikiwa ni
pamoja na kuhakikisha inawakuza wafanyabiashara wadogo na wakati
wakiwemo ‘mama lishe’.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza na mmoja wa wateja wa Benki ya NMB kushoto.
SHARE
No comments:
Post a Comment