TRA

TRA

Monday, May 29, 2017

Wenger afanya mazungumzo na Stan Kroenke juu ya mkataba mpya

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amefanya mkutano muhimu na mmliki wa klabu hiyo Stan Kroenke Jumatatu ambapo mustakabali wa mfaransa huyo ulitarajiwa kujadiliwa.

Matokeo ya mkutano huo bado hayajawekwa wazi, lakini maamuzi yanabaki baina ya Wenger na Kroenke na yatategemea pia kikao cha bodi kitakachojadili suala hilo leo hii.

 Ushindi wa kombe la FA siku ya jumamosi umekua faraja mpya kwa Wenger

Bado haijajulikana kama Wenger ataongeza mkataba baada ya kudumu katika klabu hiyo kwa miaka 21.

Masharti ya mkataba mpya yalikubaliwa miezi kadhaa iliyopita, lakini hakuna kilichofanyiwa kazi mpaka hivi sasa. 

Mipango ya Wenger ilikuwa kuendelea kubaki katika klabu hiyo lakini hali ilibadilika hivi karibuni baada ya kupingwa na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo.
Kumaliza pia nje ya timu nne bora na kukosa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao imekua changamoto kwake. 

Lakini hali kidogo imekua shwari baada ya kuifunga Chelsea 2-1 katika fainali za kombe la FA siku ya Jumamosi na kumfanya Wenger kuwa kocha mwenye mafanikio zaidi kwenye kombe hilo huku Arsenal nayo ikiwa na mafanikio zaidi kuchukua kombe hilo.

CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger