Mfanyabiashara wa
silaha, Adnan Khashoghi ambaye ni tajiri anayefahamika kwa maisha yake ya
kifahari amefariki mjini London akiwa na umri wa miaka 82.
Bwana Khashoggi alikuwa mmoja kati ya watu matajiri zaidi duniani miaka ya 1970 na 80 kwa kupata kandarasi za kimataifa za kuuza silaha.
Karamua zake zilikuwa za aina yake ambazo mara nyingi zilichukua siku kadha.
Khashoggi aliiwakilisha ufaransa katika mbioa dhidi ya Uingereza ya kushinda kandarasi ya dola bilioni 20 kuiuzia Saudi ASrabia silaha, kandarasi iliyopo hadi sasa.
Alitumikia kifungo gerezani nchini Uswisi miaka ya 1980 na kupinga kusafirishwa hadi nchini Marekani baada ya madai ya kumsaidia aliyekuwa rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos kuficha pesa.
Wakati mmoja bwana Khashoggi alikuwa mmiliki wa mashua kubwa zaidi duniani Nabila, ambayo ilitumiwa katika filamu ya James Bond ya Never Say Never Again.
Wakati biashara yake ilikumbwa na matatizo ya kifedha aliisalimisha mashua hiyo kwa Sultan wa Burnei ambaye aliiuza kwa Donald Trump ambaye sasa ni Rais wa Marekani kwa dola 29,000 miaka ya 1980.
Mfanyabiashara huyo ambaye dada yake Samira alikuwa mke wa tajiri Mohammed Al Fayed pia alikuwa mjomba wa mpenzi wa Princess Diana Dodi Fayed.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment