Waziri mkuu wa
Uingereza, Theresa May, amesema yuko tayari kubadilisha sheria yoyote ya
haki za binadamu ambayo inazuia polisi na vikosi vya usalama kupambana
ipasavyo na tishio la ugaidi.
Katika moja wapo ya hotuba zake za mwisho za kampeni, May amesema anataka kurahisisha kuzuia uhuru wa magaidi na kuwarudisha katika nchi zao za asili.
Kauli yake hiyo inafuatia shambulio la hivi majuzi lililofanyika jijini London na kuuwa watu kadhaa.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia, Julie Bishop, amethibitisha kwamba raia wa pili kutoka Australia ni miongoni mwa watu saba waliouawa katika shambulio la Jumamosi.
- Picha za aliyefanya shambulizi Manchester zatolewa
- Polisi Uingereza yamkamata mtu wa kumi
- Idara ya Usalama nchini Uingereza MI-5 kujichunguza
Raia wawili wa Ufaransa na mmoja kutoka Canada pia inaaminika kuwa miongoni mwa waliouawa.
Mjomba wa mmoja kati ya washambuliaji mwenye asili ya Pakistan ameiambia BBC kwamba analaani shambulio hilo na kwamba yuko pamoja na wanaoomboleza mauaji hayo.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment