Kundi moja la
wanaharakati wa haki za kibinaadamu nchini Tunisia limeshutumu kufungwa
jela kwa mtu aliyevuta sigara hadharani wakati wa siku ya Ramadhan.
Uamuzi huo unakiuka uhuru wa kibinafsi wa haki ya kula na kunywa katika maeneo ya uma wakati wa mwezi wa Ramadhan.
Wiki mbili zilizopita, watu wanne walihukumiwa kifungo cha mwezi mmoja jela baada ya kula katika maeneo ya uma.
- Ugonjwa wa kutopenda kula na Ramadhan
- Ramadhan na maradhi ya kutopenda kula
- Wauawa kwa bomu wakila aiskrimu, Iraq
''Mamlaka ya Tunisia haifai kuruhusu mashtaka yasiokuwa na msingi kutumika kuwahukumu raia'' ,iliongezea.''Kila mtu anafaa kuwa na haki kufuata imani zao kuhusiana na maswala ya kidini na maadili''.
Tunisia inajulikana kuwa taifa huru la Kiislamu duniani na lina umaarufu na watalii wengi kutokana fukwe zake za bahari.
Hatahivyo idadi kubwa ya raia ni Waislamu wahafidhina na wanaunga mkono sheria za Kiislamu.
SHARE
No comments:
Post a Comment