TRA

TRA

Wednesday, June 14, 2017

Aliyempiga mbunge wa Republican risasi auawa Marekani

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Polisi wakichunguza eneo la tukio

Mtu mwenye silaha ambaye aliwafyatulia risasi wabunge wa Republican wakati wakifanya mazoezi ya mchezo wa baseball mjini Washington DC ameuawa.

Kinara wa walio wengi bungeni Steve Scalise, ni mmoja wa wale waliojeruhiwa wakati wa kisa hicho cha mapema asubuhi katika hustani huko Alexandria , Virginia.

Mshambualiaji ambaye ni mzaliwa wa Illiois James T Hodgkinson, mwenye umri wa miaka 66, aliuawa baada ya ufyatulianaji wa risasi na polisi.

Waliojeruhiwa ni pamoja na polisi wawili. Hodgkinson alikuwa amemfanyia kampeni mgombea urais wa Democratic Bernie Sanders. 

Ukurasa wa Facebook ambao unaonekana kuwa wa Bwana Hodgkinsion, umejaa propaganda dhidi ya Republican na Trump.
Bwana Sanders ambaye ni Seneta wa Vermont amesema amehusunishwa na kitendo hicho cha Hodgkinson.

Rais wa Marekani Donald Trump ametaja shambulia hilo kuwa la kinyama. 

Trump alimtembelea bwana Scalise ambaye alipiwa risasi kwenye nyonga na yuko hali mahuti baada ya kufanyiwa upasuaji.

Hospitali ilisema kuwa Bwana Scalise alivunjika mifupa, na kupata majeraha ya viungo vya ndani na hivyo atahitaji upasuaji zaidi.

CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger