
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Massauni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani), kuhusu utekelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za
barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita, mjini Dodoma leo, kulia
ni Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la
Taifa la Usalama Barabarani ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia), akifafanua jambo katika
mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu hatua za utekelezaji wa mpango
mkakati wa kupunguza ajali za barabarani nchini katika kipindi cha miezi
sita, mjini Dodoma leo, kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhandisi
Hamad Massauni.

Mjumbe wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani, Mhandisi Julius Chambo (Kushoto), akisikiliza kwa
makini taarifa ya utekelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za
barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita, iliyotolewa na
Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhandisi Hamad Massauni (hayupo pichani),
mjini Dodoma leo.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Massauni, akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango mkakati
wa kupunguza ajali za barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita
kwa wajumbe na waandishi wa habari, mjini Dodoma leo.
Imetolea na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
SHARE
No comments:
Post a Comment