· Waunga mkono kampeini ya kitaifa ya usafi wa mazingira
Mashirika
ya kimataifa yanayounga mkono juhudi za serikali kuwezesha upatikanaji
wa maji safi na salama leo kwa pamoja yameunga mkono kampeni ya kitaifa
ya usafi ijulikanayo kama Niko Tayari inayoendeshwa na Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Mashirika
hayo ni UNICEF (Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto), Benki
ya Dunia, Shirika la Misaada la Uingereza (DFID), Shirika la Miradi la
Ujerumani (GIZ) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA).
Wawakilishi wa mashirika hayo walikutana kwenye ukumbi wa mikutano,
Ubungo Maji, jijini Dar es salaam leo.
Mashirika
hayo ya maendeleo yamekubali kuunga mkono kampeini hiyo ilizinduliwa
mwezi uliopita mjini Dodoma ikiwa na lengo la kuhamisha usafi wa
mazingira kwa kila Mtanzania hasa kuwa na choo katika kila familia na
kujenga utamaduni wa kunawa mikono baada ya matumizi yake. Kwa kufanya
hivyo kutasaidia kupunguza vifo hivyo kusaidia ukuaji wa uchumi nchini.
Akiongea
na waandishi wa habari, Mratibu wa kampeini ya Nipo Tayari Anyitike
Mwakitalima kutoka Wizara ya Afya alisema ili kuwa na huduma bora ya
maji, usafi wa mazingira ni muhimu kuzingatiwa. ‘Kwa kujitokeza wadau
wetu wa Maendeleo na kuunga mkono kampeini yetu ni kitu cha kupogezwa
sana na pia niishara kwamba malengo yetu ya kuwa na mazingira salama
yatafanikwa’, alisema Mwakitalima.
Zaidi ya mashirika 10 ya maendeleo ya kimataifa yamejitokeza kuunga mkono kampeini hiyo inayojumuisha mikoa yote Tanzania Bara.
Kampeini
hiyo ya usafi wa mazingira na matumizi bora ya choo (NikoTayari)
inatarajiwa kuwa chachu ya upatikanaji wa maji safi na salama na
kuboresha afya za Watanzania wote, mijini na vijijini.
Afisa Afya Mkoa wa Pwani Emmanuel Mwandepa akitoa ishara ya Nipo Tayari kuunga mkono kampeni ya taifa ya usafi wa mazingira wakati wa mkutano wa wadau wa maji uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo iko chini ya Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii ikiwa na lengo la kuhamasisha usafi wa mazingira na matumizi ya choo bora.
Mwakilishi wa TAMISEMI, Idara ya Afya, Mwajina Lipina akitoa ishara ya Nipo Tayari kuunga mkono kampeini ya Taifa ya usafi wa mazingira wakati wa mkutano wa wadau wa maji uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo iko chini ya Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii ikiwa na lengo la kuhamasisha usafi wa mazingira na matumizi ya choo bora.
Mratibu wa huduma ya maji na usafi wa mazingira shule kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Technolojia Theresia Kuiwipe akitoa ishara ya Nipo Tayari kuunga mkono kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira wakati wa mkutano wa wadau wa maji uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo iko chini ya Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii ikiwa na lengo la kuhamasisha usafi wa mazingira na matumizi ya choo bora.
SHARE
No comments:
Post a Comment