Meneja Masoko wa Benki ya Finca, Nicholous John katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa udhamini wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5 na Klabu ya soka ya Dar City F.C. Kulia ni Rais wa Klabu hiyo Azimkhan Akber Azimkhan na Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almasi Kasongo.
Rais wa Klabu hiyo Azimkhan Akber Azimkhan kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almasi Kasongo. Kushoto akizungumza katika mkutano huo.
Hapa wakitiliana saini mkataba huo.
Hapa mkataba ukiangaliwa baada ya kusainiwa.
Meneja Masoko wa Benki ya Finca, Nicholous John kushoto), akikabidhi jezi kwa Rais wa Klabu hiyo Azimkhan Akber Azimkhan kulia). Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almasi Kasongo na Makamu wa Rais wa Dar City Club, Hamidu Zuberi.
Makabidhiano yakiendelea.
Na Dotto Mwaibale
Benki
ya FINCA Microfinance leo imesaini mkataba wa udhamini wenye thamani
ya zaidi ya shilingi milioni 5 na klabu ya soka ya Dar City F.C.
Mkataba
huo uliosainiwa jijini Dar es Salaam katika makao makuu ya Benki ya
FINCA , makubaliano hayo yanajumuisha kuipatia jezi za michezo klabu
hiyo pamoja na kuipatia timu fedha za usafiri na mahitaji mengine ya
msingi katika msimu ujao wa ligi Daraja la Pili.
Akizungumza
katika hafla ya kusaini makubaliano Meneja amasoko wa FIINCA, Nicholous
John alisema kwamba udhamini huo ni kuthibitisha tena sera ya benki
hiyo ya kujikita katika kusaidia wajasiriamali vijana,
kuhakikisha wanakua na waje kuwa watu waliofanikiwa katika sekta ya
kifedha na hali kadhalika katika jamii kwa ujumla.
“FINCA
tunaamini katika kukuza umuhimu wa kukuza uchumi ndani ya jamii,
hususani vijana, na ndio maana tulikuwa tayari kukubaliana na juhudi
za ziada za vijana hawa baada ya kubaini kwamba wanavyo vipaji vya
kuwawezesha kufika mbali kulingana na hali ya michezo ilivyo,” alisema
John na kuongeza kwamba wameamua kujumuisha utamaduni wa ujasiriamali
katika michezo.
Dar
City FC ambayo ilifanikiwa kuingia katika mashindano ya Kombe la
Mabingwa wa Shirikisho hivi karibuni inatarakiwa kusafiri hadi Kahama,
mkoani Shinyanga ambako itaungana na timu nyingine saba katika ligi
ya mabingwa wa mikoa nchini.
Aidha
Rais wa Klabu hiyo Azimkhan Akber Azimkhan aliishukuru FINCA kwa
ukarimu huo wa msaada akisema kuwa umekuja wakati sahihi na katika
kipindi ambacho klabu hiyo inakabiliwa na changamoto za kifedha.
“Tunatoa
shukrani nyingi kwa Benki ya FINCA kwa msaada huu uliokuja kwa wakati
mwafaka, sasa hivi tuna uhakika kwamba tutafanya vizuri katika
mashindano kwa kuwa udhamini huu utatuwezesha kwa kiwango kikubwa kwa
timu kuwa na morali na hamasa ya kufanya kazi kwa bidii, “ alisema
Azimkhan.
Alifafanua
kuwa matayarisho kwa ajili ya mashindano hayo yanajumuisha mahitaji
kadhaa na hiyo ni changamoto kwa makampuni mengine, watu binafsi na
mashirika katika kuzisaidia timu zinazoibua kwa kutambua umuhimu wake.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA),
Almasi Kasongo wakati akiishukuru FINCA kwa udhamini wake alitoa wito
kwa taasisi nyingine za kifedha kuiga mfano maridhawa wa FINCA kwa
kuzisaidia klabu nyingine za soka zinazoibukia ndani ya jiji.
SHARE
No comments:
Post a Comment