Bingwa wa ndondi za uzani mzito duniani anayeshikilia taji la WBC Deontay Wilder ameshtakiwa kwa kumiliki bangi.
Maafisa wanasema kuwa walipata dawa hiyo ndani ya gari lake.
- Wabunge waidhinisha kilimo cha bangi
- California yaidhinisha matumizi zaidi ya bangi
- Marekani yaamua: Trump, Clinton na Bangi
- Canada kuhalalisha bangi ifikapo mwaka ujao
Aliambia chombo hicho kwamba Deontay amekuwa safarini kwa siku kadhaa.
Alirudi nyumbani leo kutoka Georgia akiwa anaendesha gari lake la Rolls Royce na kuchukua gari jingine aina ya Cadillac Escalade kutembea maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.
Wilder alishtakiwa na polisi na kuachiliwa huru kwa dhamana ya dola 1000.
Maafisa walipata ruhusa ya kulisaka gari hilo kabla ya kufanikiwa kupata kiwango cha bangi kutoka kwa gari hilo, taarifa ya maafisa wa polisi wa Tuscaloosa ilisema.
Pigano la mwisho la Wilder lilikuwa la ushindi wa raundi ya tano kwa njia ya Knockout dhidi ya Gerlad Washington alipotetea taji lake la WBC ambalo amemiliki tangu 2015.
SHARE
No comments:
Post a Comment