TRA

TRA

Wednesday, June 14, 2017

Dodoma kinara mimba za utotoni

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Anthony Ishengoma- Dodoma
 
Takwimu zinaonyesha kuwa Mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa mimba na ndoa za utotoni ambapo asilimia ya wasichana wenye miaka kati ya 20 -22 walioolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18 kwa mkoa wa Dodoma ni asilimia 51 ukilinganisha na asilimia 37 ya kitaifa.
 
Hayo yamesemwa na Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Tafma Touwfiq wakati uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoanza jana mkoani Dodoma.
Wanafunzi kama hawa wanahitaji kulindwa
Akiongea katika uzinduzi huo mjini Dodoma Mbunge huyo amesema kwa takwimu hizi maana yake ni kwamba kati ya watoto 100, watoto 51 wanaoolewa kabla ya kufikia miaka 18.
 
Ameongeza kuwa watoto wanaozaa wakiwa na umri mdogo ni asilimia 39 akizitaja taakwimu hizi kuwa zinaonyesha tunahitaji kuongeza jitihada na kuwekeza Zaidi katika mikakati yetu ya kumuwezesha na kumuendeleza mtoto wa kike.
 
Bi. Tafma amewambia wadau wa maendeleo ya mtoto wa kike katika mkoa wa Dodoma kuwa Mkoa umezinduwa kampeni ya kupambana na ndoa na mimba za utotoni na kampeni hii ni kubwa na itaendelea hadi tutakapofikia malengo ya kumkomboa mtoto wa kike na kumuweka katika mazingira salama ya kumuwezesha kufikia ndoto zake.
 
Ili kuonesha mkakati wa kupambana na ndoa za utotoni mkoani Dodoma Mbunge huyo amesema mkakati unaotumiwa kwasasa ni ule ujalikanao kama magauni manne akiyataja magauni hayoa kuwa gaunai la kwanza ni kuhimiza mtoto wa kike kuwa ndani ya sale ya shule, gauni la pili ni nilile la kuhitimu masomo na la tatu ni gauni la harusi na lakutiza ndoto ni gauni wakati wa ujauzito mtoto wa kike akiwa ametimiza ndoto zake.
 
Maadhimisho hayo yanaendelea mjini Dodoma katika ngazi ya mkoa na kaulimbiu ya mwaka huu inasema; “Maendeleo Endelevu 2030: Imarisha Ulinzi na Fursa sawa kwa Watoto”.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger