Shirikisho
linaloweka sheria za soka duniani lina mpango wa kupunguza muda wa
kipindi cha kwanza na cha pili cha mchezo ili kuwa dakika 30.
Waliopendekeza mpango huo wanasema kuwa mechi huchezwa kwa dakika 60 pekee kati ya tisini na muda uliosalia hutumiwa kupoteza wakati.
Wanapendekeza dakika 30 kila kipindi huku muda ukisimamishwa kila mpira unapotoka kusaidia kukabiliana na muda unaopotezwa mbali na kuufanya mchezo kuvutia zaidi.
Mshikemshike uwanjani
Wakosaoji wanasema kuwa mabadiliko kama hayo hayatakuwa na umuhimu wowote iwapo sheria ya kupoteza muda itaimarishwa.
- Fifa kuanza kutumia Video michezoni
- Sheria mpya Indonesia 'itamaliza visa vya unajisi'
- Wanaotafuta baba za watoto wao,kutaja waliofanya mapenzi nao Ujerumani
Na iwapo penalti hiyo haikupigwa ilivyotarajiwa ,mchezo utasitishwa na mpira wa adhabu kutolewa.
Mapendekezo mengine yanashirikisha kuweka saa katika uwanja ambayo italingana na ile ya refa mbali na sheria mpya itakayoruhusu mchezaji kujipigia mpira ama hata kutamba na mpira wakati anapopiga mpira wa adhabu.
Tayari aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Gianfranco Zola anapendelea pendekezo hilo la kupunguza muda wa dakika za mechi hadi 60.
SHARE









No comments:
Post a Comment