Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akisitiza jambo kwa wadau walioshiriki
zoezi la usafi katika fukwe ya bahari ya Hindi eneo la Aga Khan na
kuwaomba waendelee na kufanya usafi na hata kuwahamasisha watu wengine
kuwa mabalozi wa mazingira ili kufikia malengo waliyojiwekea katika
manispaa ya Ilala.
Baadhi
ya wadau wa mazingira waliofika kwenye zoezi la usafi katika wiki ya
Mazingira lililoendeshwa na kampuni ya Green Waste Pro Ltd wakimsikiliza
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema.
Naibu
Meya wa Manispaa ya Ilala , Mstahiki Omary Kumbilamoto akizungumza
jambo kwa wadau mbalimbali waliokuja kujumuika katika zoezi la usafi
katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Agha Khan katika wiki ya
mazingira.
Meneja
wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste ProLtd, Abdallah Mbena
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa kampuni hiyo
katika zoezi la kufanya usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya
Kivukoni eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira.
Wafanyakazi
wa Manispaa ya Ilala pamoja na wafanyakazi wa Green Waste Pro
Ltd wakiendelea kufanya usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya
Kivukoni eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira. Mwenye
shati nyeupe ni Meneja Msaidizi wa kampuni Green WastePro ltd, Erick Mark.
Baadhi
ya wadau wa mazungira wakifanya zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari
ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki
ya Mazingira huku akishirikiana na viongozi wa kampuni iliyopewa zabuni
ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd pamoja na wafanyakazi
wa manispaa ya Ilala.
Baadhi
ya uchafu ukiwa kwenye mifuko yake mara baada ya kumalizika kwa zoezi
la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya
Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira huku akishirikiana na
viongozi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala
Green Waste Pro Ltd pamoja na wafanyakazi wa manispaa ya Ilala.
SHARE
No comments:
Post a Comment