Emir
wa Qatar Thamim Bin al-Thani akisalimiana na Rais wa Marekani Donald
Trump huko Saudi Arabia mwezi uliopitaTaharuki ya Qatar na majirani
zake, inaendelea kuongezeka, licha ya wito wa mazungumzo kutolewa.
Safari za
ndege zinazotoka Qatar kuelekea Saudi Arabia, Misri na Bahrain
zimefutiliwa mbali kuanzia siku ya Jumanne.Mataifa kadhaa tayari
yamekomesha uhusiano wao na kidiplomasia na taifa hiolo lililoko katika
rasi ya Arabia, huku yakililaumu kwa "kuunga mkono ugaidi". Doha
inakatalia mbali shutma hizo.Mwaandishi wa BBC wa idhaa ya Kiarabu Amir
Rawash, anatathmini namna taharuki kati ya Qatar na majirani zake
imefikia kiwango cha kutamausha.Emir wa Qatar Thamim BIn al-Thani
Kundi la Muslim Brotherhood
Baraza la
ushirikiano wa mataifa ya ghuba, yanasema kuwa Qatar iliunga mkono
upinzani wakati wa vuguvugu lililotokea kwa mataifa ya kiarabu.Doha,
ilionekana kama muungaji mkono wa makundi ya kiislamu, ambayo ilitaka
kupata umaarufu katika baadhi ya mataifa ya kiislamu.Kwa mfano, baada ya
kuondolewa kwa Rais wa Misri Mohamed Morsi - kinara mkuu wa Muslim
Brotherhood - ambaye alitimuliwa mamlakani mwaka 2013, Qatar iliwapa
hifadhi wanachama wa kundi hilo ambalo limepigwa marufuku na utawala wa
Misri.Saudi Arabia na Milki za kiarabu UAE pia zilitaja Muslim
Brotherhood kama kundi "la kigaidi".Katika taarifa iliyochapishwa katika
mtandao rasmi wa habari za utawala wa serikali ya Saudia, Qatar
ililaumiwa kwa "kuzikubalia makundi kadhaa ya kigaidi na makundi yenye
itikadi kali yenye nia ya kuyumbisha amani katika kanda ya mataifa ya
kiarabu, kwa pamoja na makundi kama la Muslim Brotherhood, Daesh (Isis)
na Al-Qaeda".Hata hivyo, Wizara ya nchi za nje ya Qatari, ilisema kuwa
hatua zilizochukuliwa na Riyadh, Abu Dhabi na Manama "hazikuridhisha na
yanaegemea madai yasio na msimamo kabisa wala ukweli".TTaaarifa hiyo
aidha inasisitiza kuwa, Qatar inafaa "kujitolea " chini ya mkataba wa
GCC na "kutekeleza majukumu yake ya kukabiliana na ugaidi na itikadi
kali".
Mbinu ya
IranMzozo wa sasa ulianzishwa na taarifa iliyokataliwa iliyomnukuu Emir
wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani, akikosoa "uadui" wa Marekani
dhidi ya Iran.Qatar ilisema kuwa wadukuzi wanatazamiwa kuchapisha maoni
hayo katika shirika lake la habari la taifaSaudi Arabia, mpinazi mkuu wa
taifa hilo la kiislamu, limekuwa likitatizwa kwa muda mrefu na umaarufu
wa Iran katika kanda hiyo.
Mzozo nchini Libya
Libya
imekuwa katika lindi la mzozo tangua kuangushwa kwa utawala wa Rais wa
nchini Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.Kiongozi mkuu wa jeshi ya Libya
Khalifa Haftar, ambaye alipata uungwaji mkubwa kutoka Misri, Milki za
kiarabu UAE na Qatar, aliilaumu Qatar kwa "kuunga mkono ugaidi".Haftar
anaongoza serikali iliyoko mashariki mwa Libya katika mji wa Tobruk.
Ilihali Qatar inaunga mkono serikali pinzani iliyoko katika mji mkuu
Tripoli.Emir of Qatar wakati wa kongamano la mataifa ya kiarabu huko Saudi Arabia mwezi uliopita
Mzozo wa vyombo vya Habari
Mara tu
taarifa tatanishi ilipotolewa ikimnukuu Emir wa Qatar mnamo Mei 23,
vyombo vya Habari huko UAE, Saudi Arabia, Bahrain na Misri yalianzisha
ukosoaji mkubwa dhidi ya familia inayotawala Qatar.Mataifa hayo manne
yaliamua kwa kauli moja kuzima mtandao wa habari wa Qatar.Jumanne jioni
Rais wa Marekani Donald Trump aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii
wa Tweeter kuwa kushindwa kwa Qatar, itakuwa mwanzo wa kumalizika kwa
makundi ya kigaidi duniani.
SHARE
No comments:
Post a Comment