Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni William Makufwe awashukuru
BAY PORT Taasisi ya kifedha kwa msaada wa kompyuta mbili walizozitoa
Jana kwa Idara ya Utumishi na Rasilimali watu..
Mkurugenzi
Mtendaji alisema kuwa anashukuru kwa msaada wa kumpyuta hizo ambazo
zitakwenda kwenye Idara ya Utumishi na Rasilimali watu ili kuimarisha
Idara na ufanisi wa Idara hiyo kwa kuzingatia unyeti wa eneo hilo na
huduma wanayoitoa kwa watumishi.
Miongoni
mwa Halmashauri 80 ambazo zimelenga kufikiwa na BAYPORT tunashukuru
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imekuwa moja wapo na tunaahidi kutumia
vifaa hivi vya TEHAMA kwa kuongeza ufanisi na utendaji kazi ulioboreka
zaidi.
Mratibu
wa masoko na mawasiliano wa huduma za kifedha za BAYPORT Mercy Ndunguru
alisema kuwa BAYPORT imeamua kurudisha faida ambayo wameipata ambapo
kwa sasa wameona waguse sekta ya utumishi ambayo imekuwa na msaada
mkubwa katika kufikia malengo.
Mercy
alisema kuwa, Tunaamini kwa kutoa vifaa hivi vya TEHAMA itasaidia
kuongeza ufanisi kwenye sekta ya utumishi na watumishi watapata huduma
kwa wakati, BAYPORT inamuunga mkono Raisi kwenye utendaji kazi kwa
watumishi.
Meneja
wa BAYPORT Handeni Kanji Masanji alisema kuwa, anashukuru kwa
ushirikiano anaoupata kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na
kwamba taasisi yao inajipanga kufanya mambo mengine makubwa zaidi ya
haya ikiwa ni pamoja na kujipanga kufadhili timu mbalimbali za mipira na
kuinua vipaji vya vijana waliopo Wilayani Handeni.
BAYPORT
wametoa msaada huo wa kompyuta mbili ikiwa ni miongoni mwa kompyuta
zenye thamani ya zaidi ya milioni 500 zinazoendelea kutolewa kwenye
taasisi nyingine za Kiserikali.
Alda Sadango
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni William Makufwe kushoto akipokea Msaada wa kompyuta kutoka Kwa Mratibu wa masoko na mahusiano kutoka BAYPORT Mercy Ndunguru.
Afisa utumishi Wilaya Noel Abel akipokea Msaada wa kompyuta kutoka Kwa Mratibu wa masoko na mahusiano kutoka BAYPORT Mercy Ndunguru.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ambapo kushoto ni Afisa utumishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na kulia ni Mratibu wa masoko na mahusiano na meneja wa tawi LA BAYPORT Handeni
SHARE
No comments:
Post a Comment