Na Benjamin Sawe.
Maelezo
Upo usemi wa wahenga usemao “mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.”
Hivi ndivyo ninavyoweza kusema kuhusiana na harakati za Serikali ya
Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
katika kuhakikisha kuwa Sekta ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi
inaimarika.
Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya
kuteuliwa kuwa Rais, amekuwa Waziri katika Awamu mbili zilizopita. Anao
uzoefu mkubwa wa utendaji kazi lakini pia katika kuongoza Wizara ambapo
amewahi kuwa Waziri wa Ujenzi na Miundombinu na Kilimo na Ufugaji.
Kutokana na umuhimu wa Sekta ya
Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi katika maendeleo ya Taifa, mara tu baada
ya kuchaguliwa kuwa Rais, aliagiza ujenzi wa barabara ya kutoka Mwenge
hadi Moroco ambayo ilikuwa ina msongamano mkubwa wa magari kuelekea
katikati ya jiji.
Msongamano huo umekuwa ukiathiri
malengo ya Wafanyakazi ambao walikuwa wakitumia muda mwingi wakiwa
kwenye foleni na hivyo kupunguza muda wa kufanya kazi lakini pia
uzalishaji na utoaji huduma za msingi kwa Taifa.
Aidha, Mheshimiwa Rais ameshiriki
uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa barabara za juu (fly
over) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela eneo la Tazara
unaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 100 za Kitanzania na pia ujenzi
wa barabara za juu kwenye makutano ya barabara za Morogoro, Mandela na
Sam Nujoma eneo la Ubungo Jijini Dar es Salaam
Hivi karibuni Serikali kupitia
Waziri Mwenye dhamana ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Prof. Makame Mbarawa amepokea Kivuko cha MV Kazi ambacho kimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya M/S Songoro Marine Transport Boatyard ya Mwanza.
Kivuko hicho kilichogharimu jumla
ya Shilingi bilioni 7.3 za Kitanzania, ni moja ya ahadi ya Mheshimiwa
Rais John Magufuli alizozitoa wakati wa Kampeni zake za Urais za
kuwapunguzia kero za usafiri Wananchi wakiwemo wakazi wa Kigamboni.
Akipokea Kivuko hicho chenye uwezo
wa kubeba abiria 800 na magari 22 Prof. Mbarawa amesema lengo la
Serikali ni kuboresha huduma za kusafirisha abiria na magari kati ya
Magogoni na Kigamboni ambapo kwa muda mrefu kimekuwa kilio cha Wananchi
waishio kigamboni.
Kabla ya ujio wa kivuko hicho
kipya kumekuwa na jitihada zizolikuwa zinafanywa na Serikali katika
kutatua tatizo la usafiri kwa Wananchi wa Kigamboni kwa njia ya Pantoni.
Moja ya jihihada katika kukabiliana na tatizo hilo ni ujenzi wa Kivuko cha MV Magogoni chenye uwezo wa kubeba abiria 2000 na magari 60 kwa pamoja sawa na Tani 500.
Profesa Mbarawa amesema Kivuko cha
MV Kazi kinakwenda kuimarisha usafiri kwa Wakazi wa Kigamboni ambapo
kwa sasa kutakuwa na jumla ya Vivuko vitatu kikiwemo pia kivuko cha…..
Aidha, uzinduzi wa daraja la
Kigamboni ni moja ya mafanikio makubwa ambayo yanafanywa na Serikali ya
Awamu ya Tano inayotekeleza Ilani yake ya Chama Tawala cha CCM.
Daraja hilo licha ya kuunganisha
wananchi wa Kigamboni lakini pia linaunganisha watu wote ikiwa ni pamoja
na kuleta maendeleo nchini hasa kwa wakazi wa Kigamboni.
Daraja la Kigamboni lenye urefu wa
mita 680 linaunganisha upande wa Kurasini na Kigamboni wenye urefu wa
Kilometa 2.5. Ujenzi wa daraja hilo umefanywa na Kampuni ya China
Railway 15 Group ikishirikiana na Kampuni ya China Bridge Engineering
Group na umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 250 za Kitanzania.
Kwa maoini yangu, utendaji wa
jinsi hii unatoa taswira ya uwajibikaji mahsusi unaopaswa kufanywa na
viongozi wa Kisiasa ukihusisha usimamizi na ufuatiliaji yakinifu wa
Sera/michakato/mikakati na mipango ya serikali.
Usimamizi na ufuatiliaji
unaofanywa na Prof. Mbarawa uwe chachu kwa Viongozi wengine wa Serikali
na Wanasiasa waliopewa dhamana katika awamu ya Tano. Si jambo geni
kumsikia Prof. Mbalawa kwa siku moja akiwa katika mikoa miwili tofauti
akifuatilia utekelezaji wa ahadi za Serikali ya Awamu ya Tano.
Wapo watu wanaoweza kubeza
uwajibikaji wa Waziri huyu lakini kimsingi anachofanya ni kuhakikisha
kuwa Wananchi wanapata huduma ya msingi katika kuwaletea maendeleo yao
na Taifa kwa jumla. Ndio maana nimesema kuwa “mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.”
SHARE
No comments:
Post a Comment