Malkia wa Uingereza
anatarajiwa kupokea asilimia 8 ya nyongeza ya mshahara kutoka kwa
fedha za umma baada ya biashara ya ufalme huo kupata faida iliopanda kwa
pauni milioni 24.
Inajiri huku akaunti zikionyesha kuwa matumizi ya malkia mwaka uliopita yalipanda kutoka pauni milioni mbili hadi pauni miolini 42.
Alan Reid ambaye ni msimamizi wa fedha hizo alisema kuwa Malkia aliwakilisha utumizi mzuri wa fedha.
Ufadhili huo unatolewa kila bada ya miaka miwili ,ni fedha anazopewa malkia na wizara ya fedha.
Zinatokana na faida za biashara za malkia ambazo zinashirikisha eneo kubwa la West End mjini London.
Biashara hizo zilimpatia malkia faida ya pauni milioni 24.7 hadi pauni milioni 328.8 mwaka 2016/17
SHARE
No comments:
Post a Comment