Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
akisalimiana na viongozi wa vituo nane vya kulelea yatima na watoto
wanaoishi kwenye mazingira magumu kabla ya kuwakabidhi vyakula kwa ajili
ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na sikukuu ya Eid el Fitr Ikulu
jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017.
Mke wa Rais
Mama Janeth Magufuli akimkabidhi Hajat Mwanaisha Magambo mkuu wa kituo
cha New Life Orphanage cha Boko Dawasco kwa niaba ya viongozi wa vituo
nane vya kulelea yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu
waliopewa vyakula kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na
sikukuu ya Eid el Fitr na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli Ikulu
jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017. Vituo vilivyopkea vyakula hivyo
ni pamoja na New Life kilichopo Boko Dawasco chanye watoto 121,
Charambe Islamic kilichopo Charambe (watoto 54), Mwandaliwa Centre
kilichopo Mbweni (watoto 94) Al Madina Children Home cha Tandale (
watoto 65), Ijangozaidia Orphanage Centre kilichopo Sinza (watoto 1030,
Azam Orphanage kilichopo Mbagala (watoto 51), Hiari Orphanage kilichopo
Chang’ombe (watoto41) na CHAKUWAMA (watoto 64) kilichipo Sinza.
Mke wa Rais
Mama Janeth Magufuli akimsabahi mmoja wa yatima maaba ya kumkabidhi
vyakula Hajat Mwanaisha Magambo kutoka kituo cha New Life Orphanage cha
Boko Dawasco kwa niaba ya viongozi wa vituo nane vya kulelea yatima na
watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu waliopewa vyakula kwa ajili ya
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na sikukuu ya Eid el Fitr na Mke wa
Rais Mama Janeth Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 20, 2017
PICHA NA IKULU
SHARE
No comments:
Post a Comment