Mchezaji wa
Argentina amesababisha rabsha baada ya kukiri kwamba alitumia sindano
kumdhuru mpinzani wake katika mechi ya kuwania kikombe siku ya Jumapili.
Allende amesema wachezaji walihitaji kuwa werevu ili kupata ushindi. Rais wa shirikisho la soka la Pacifico Hector Moncada ameapa kumfukuza mchezaji huyo.
''Tumekasirishwa sana. Kisa hicho kimeharibu kazi nzuri ya timu . Nitamfukuza kutoka kwa klabu.'' Bw Moncada aliambia gazeti la Clarín.'
Pacifico ilishinda mechi hiyo kwa magoli 3-2 na kuibandua Estudiantes nje ya mashindano kwa uchungu mkubwa.
Wachezaji hao walikaribishwa nyumbani kama mashujaa katika mji mdogo wa magharibi wa Jenerali Alvear waliporudi kutoka Buenos Aires, pale mechi ilipochezwa.
'Lazima atanichukia'
Mandhari mazuri yalibadilika na kuwa habari mbovu.Allende alikubali kuhojiwa na kituo cha radio cha Cordoba's Vorterix siku ya Jumanne aliposema lazima ucheze vibaya'' ili kuzishinda timu kubwa kama Estudiantes de La Plata.
Nilikuwa nikimdunga mshambuliaji wa Estudiantes na sindano , amesema beki huyo wa Pacifico.
''Tunafahamu kwamba wachezaji wa daraja la juu hawapendi kuguswa , hawapendi kupoteza wakati ama ukiwachezea vibaya. Sasa hiyo ndio ilikuwa mbinu bora ya kutumia. Soka ni ya watu werevu,'' Allende amesema.
Mtaalam wa soka kutoka Afrika Kusini, Tim Vickery aliambia BBC, Allende alikuwa ameficha sindano mbili katika mavazi ya kuvaa miguuni . lakini sindano moja ilivunjika , wakati muamuzi wa mchezo huo alipokuwa upande mwengine , Allende alitumia sindano nyengine kumdunga mshambuliaji wa Colombia Juan Otero mara Kadhaa.
Otero alimlalamika kwa muamuzi wakati mechi hiyo ikiendelea lakini aliangulia patupu.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment