Meya
mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda amewataka wananchi,
taasisi na viongozi mbalimbali wenye uwezo kuwasaidia watoto wanaoishi
katika mazingira magumu kwa lengo la kuwakwamua na hali ya kiuchumi
iliyopo kwa sasa.
Mwenda
ameyasema hayo Jijini Dar es salaam jana katika hafla ya Idd aliyoindaa
nyumbani kwake na kusheherekea na watoto yatima wanaolelewa katika
kituo cha Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni.
Alisema
pamoja na mambo mengine,kufanya hivyo ni kumuunga mkono Rais John Pombe
Magufuli katika harakati zake za kimaendeleo anazozifanya.
Alisema
viongozi wananchi pamoja na jamii kwa ujumla haina budi kuendana na
dhamira aliyonayo Rais Magufuli ya Taifa kujikwamua kiuchumi hususani
kipindi hiki anapofanya mambo mbalimbali ya kuliletea maendeleo.
"Huu
ni watati wa kila mmoja wetu kujitafakar, watoto hawa si yule mzazi
aliyewazaa, bali wa taifa zima, hivyo ni vyema kila mmoja wetu akaona
umuhimu wa kuwalea watoto hawa kiakili na kimaadili" alisema Mwenda.
Aidha
alisema viongozi waliopo madarakani kwa pamoja wanapaswa kushirikiana
pamoja kuhakikisha maendeleo ya nchi hii yanapatikana kwa kasi huku
akisisitiza kuwa pasipo ushirikiano huo hakuna maendeleo hayo yanayoweza
kupatikana.
Awali
Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa hiyo Prosper Mosha aliwataka wananchi
mbalimbali wa manispaa hiyo kujitokeza kusaidia malezi ya watoto
walioko vituoni kufuatana na utaratibu uliowekwa na manispaa hiyo.
Alisema
Manispaa hiyo imeweka utaratibu wa kila anayehitaji kulea mtoto
anayeishi katika miongoni mwa vituo vya watoto yatima, kupewa mtoto
anayemuhitaji kwa lengo la kumlea.
"kwa
sasa utaratibu upo wazi, kila anayehitaji kupata mtoto wa kumlea
anapaswa kuja ofisini ili apate maelezo, ila utaratibu upo wazi kabisa
kikubwa ni uzingatiaji wa sheria tulizoziweka" alisema Mosha.
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akizungumza wakati wa hafla ya Idd aliyoindaa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. na kusheherekea na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni .
Mratibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Imra James Gabon akitoa neno la shukrani mara baada ya kupokea msaada.
Afisa
Ustawi wa Jamii wa Manispaa hiyo Prosper Mosha akizungumza.
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akiwakabidhi watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni .baadhi ya zawadi aliyowaandalia (kushoto) Mratibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Imra James Gabon.
Mke wa Meya Mama Tausi Yusufu Mwenda (mwenye nguo ya bluu) akimkabidhi moja ya zawadi Bi.Nuhimu Iddi anayetoka katika kituo hicho.
Watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni .
Shampeni ikifunguliwa.
Wageni waalikwa wakipata shampeni.
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akipata shampeni.
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akipata shampeni.
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akiwaongoza watoto kupata chakula.
Watoto
yatima wanaolelewa katika kituo cha Umra kilichopo Magomeni katika
Manispaa ya Kinondoni wakisherekea siku ya Iddi nyumbani kwa Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda.
Wageni waalikwa.
Mc aliyeandaliwa kwaajili ya sherehe hiyo akisisitiza jambo.
Airtel yafuturisha wafanyakazi wake siku ya ijumaa kabla ya sikukuu ya Eid
Wafanyakazi
katika kitengo cha mawasilino cha Airtel wakiwa katika picha ya pamoja
kabla ya kufuturu . kushoto ni mkurugenzi wa mawasiliano Beatrice
Singano, akifatiwa na Afisa uhusiano Jane Matinde, Meneja huduma kwa
jamii, Hawa Bayumi pamoja na Afisa uhusiano na matukio, Dangio Kaniki
Sheikh Hilal Kipoozeo akiongoza wafanyakazi wa Airtel pamoja na baadhi ya wageni kwenye futari
Wafanyakazi wa Airtel pamoja na baadhi ya wageni kwenye futari
Wafanyakazi wa Airtel pamoja na baadhi ya wageni kwenye futari
Wafanyakazi wa Airtel pamoja na baadhi ya wageni kwenye futari
Wafanyakazi wa Airtel pamoja na baadhi ya wageni kwenye futari
Wafanyakazi wa Airtel pamoja na baadhi ya wageni kwenye futari
Sheikh Hilal Kipoozeo akitoa mawaidha kwa walioshiriki futari iliyoandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
Wafanyakazi wa Airtel pamoja na baadhi ya wageni kwenye futari
Wafanyakazi wa Airtel pamoja na baadhi ya wageni kwenye futari
Wafanyakazi wa Airtel pamoja na baadhi ya wageni kwenye futari
SHARE
No comments:
Post a Comment