TRA

TRA

Tuesday, June 13, 2017

MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO KATIKA ZIARA YA MAFUNZO NCHINI UFARANSA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akikaribishwa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Samwel Shelukindo katika ubalozi uliopo jijini Paris.  Gambo yupo katika ziara ya mafunzo nchini Ufaransa, ambapo pamoja na mafunzo hayo amekuwa akiutangaza mkoa wa Arusha kama kitovu cha utalii nchini Tanzania. 

Mhe Gambo akiwa huko mefanya mazungumzo na Balozi Shelukindo, na kubadilishana mawazo ya namna ya kuvutia wananchi wa nchi hiyo kutembelea Tanzania. 

Ufaransa ni moja ya zinazoleta watalii wengi nchini Tanzania. Pamoja na mambo mengine  Mhe RC na Balozi wamejadiliana mambo ya Msingi ya kufanya ili kuongeza watalii kutoka Ufaransa kuja Arusha, kupata wawekezaji kutoka Ufaransa kuja Arusha pamoja na namna ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Mkoani humo, pamoja na kuanzisha tukio la kimataifa la kutangaza utalii mkoani Arusha kila mwaka.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akiweka saini katika kitabu cha wageni baada ya kukaribishwa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Samwel Shelukindo katika ubalozi wetu uliopo jijini Paris.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger