TRA

TRA

Monday, June 19, 2017

Nyumba zinazotajwa kuwa za ajabu kuelea kwenye maji

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Kila siku duniani kunafunguliwa hoteli, sehemu za starehe na sehemu za mapumziko zenye upekee kulingana na mazingira na namna ya kuvutia watu ili kukuza biashara.

Leo June 18, 2017 nimekusogezea nyumba tatu zinazoelea kwenye maji ambazo ni maalumu kwa ajili ya mapumziko.

Floating Summer House

Nyumba hii ina ghorofa mbili ambayo inapatikana Canada kwenye Ziwa Huron. Nyumba hii hutumika kama makazi ya majira ya joto kwa wapenzi wenye asili ya Cincinnati. Ilimalizika ujenzi wake mwaka 2008 ikiwa ni moja ya projects za mwanzo za MOS Architects



Belgrade apartments

Hizi ni hostel na apartments ambazo zinaitwa ArkaBarka zipo katika ukingo wa Mto Danube, Belgrade. 

Katika jengo hili ambalo huelea kwenye maji lina mambo mengi ya anasa vikiwemo sauna na bar. Zimejengwa kwa kiwango cha hali ya juu ambapo vyumba vyake vinaanzia euro 25.50 na bei zote hujumuisha breakfast na WiFi.


Maldives floating house

Maldives Floating House ilibuniwa na msanifu wa majengo wa Singapore anayeitwa Dymitr Malcew. Kwa mujibu wake ni kuwa alitaka kutengeneza kitu ambacho kitawaruhusu watu kuukubali uhuru na asili. 

Nyumba ina vyumba viwili vya kulala, vyoo viwili, chumba cha kupumzika na jiko. Nyumba hii ina uwezo wa kusogea kutoka sehemu moja hadi nyingine.


 

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger